Loading...

Chelsea wamekamilisha taratibu za usajili wa beki huyu wa Ujerumani


Kabla ya kukamilisha dili la Timoue Bakayoko na Alex Sandro, Chelsea tayari wamekubali kulipa kiasi cha paundi milioni 34 kukamilisha uhamisho wa Antonio Rudiger kutoka Roma.

Kwa mujibu wa taarifa ya 'Sky Sports', uhamisho huo tayari umekwisha kamilika.

Mjerumani huyo atafanyiwa vipimo vya afya huko Los Angeles wiki hii kabla ya kutambulishwa rasmi kama mchezaji wa 'The Blues'. Beki huyo anawatangulia Timoue Bakayoko na Alex Sandro ambao nao inaonekana wako katika hatua nzuri kusainiwa na Chelsea katika dirisha hili la usajili.

Rudiger anaweza kucheza katikati au katika upande wowote kwenye mfumo wa 3-5-2 unaotumiwa na kocha Antonio Conte.

Inaeleweka kwamba Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Uingereza wamekubali kulipa kiasi cha karibuni paundi milioni 36 kwa ajili ya Rudiger lakini, aliwahi kuweka wazi kuwa, yeye ni mshabiki wa siri wa Arsenal ambao ni mahasimu wakubwa wa Chelsea pale London.

Itabakia kusubiri kama ataweza kuhimili mapigo mapya katika Ligi Kuu ya Uingereza, lakini kwa Chelsea watakuwa na furaha sana kukamilisha usajili huo.
Chelsea wamekamilisha taratibu za usajili wa beki huyu wa Ujerumani Chelsea wamekamilisha taratibu za usajili wa beki huyu wa Ujerumani Reviewed by Zero Degree on 7/07/2017 07:10:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.