Loading...

Fumanizi la Mapenzi: Sehemu ya 11


MTUNZI: MC Short Charles Gwimo

Ilipoishia.........Nilimwambia, “Endapo utaulizwa kulikoni, uwape majibu haya, ….nina tatizo la mguu ambao nilikwatuliwa ngwara na kijana nisiyemfahamu nilipomkatalia ombi lake la kucheza naye muziki….” “Kijana huyo sikumfahamu vizuri kwani alikuwa amevalia boshori ili kuficha uso wake” ……Nilimpeleka bwenini ili apumzike. Tulipoachana nilipiga ngumi hewani kama ishara ya ushindi kwa kuua tembo kwa ubua. Niliitoa shajara yangu ndogo na kuandika kumbukumbu ya tukio hilo ili ibakie historia ya uzinduzi wa mapenzi kwa kufanya mapenzi kwa mara ya kwanza na gashi mwenye kizinda. Sijui wewe mwenzangu una historia gani kwenye mahusiano. Nakuomba ujikumbushe ili upate kujichekea.

Endelea nayo: Disko lilifungwa mnamo saa 8:30 usiku huku kila mtu akielekea mabwenini kujipumzisha. Usiku huo hakukuwa na masimulizi mema zaidi ya kuzungumzia mwenendo mzima wa disko na uchafu uliofanyika kwa baadhi ya wanafunzi. Kulikuwa na makundi matatu yaliyojisifu kufaidi disko kwa kiwango stahiki na wengine rasharasha kama mvua za vuli. Kundi la kwanza ni lile ambalo lilicheza muziki na hatimaye kulishwa kipapai baada ya kunogewa kwa blues zilizochezwa kwa mfululizo, na la pili ni lile la waliolishana kiboga wenyewe kwa wenyewe likiwa limesheheni mabasha wazoefu kama walivyojinadi na kundi la mwisho ni lile la wale waliomla samaki pande zote, na hapa nammaanisha kundi lililokutana na wanajamii wa Mombasa au wa zama za Sodoma na Gomora wanaohusudu kuruka ukuta au kupitia mlango wa buti na kumalizia lango kuu la Edeni. Kuna waliojisifu kunyonywa chururu zao na wengine kunyonya hadi chumvini huku ncha ya ulimi ikijisumakisha sambamba na ncha ya kinyama hisia kilichopo katikati ya vijaruba vya mbele vya mtoto wa kike ambako ndugu zangu wakulia hukifanyia tohara wakiamini kuwa huo ndiyo usafi sahihi kwa mtoto wa kike ilihali ni mila potofu na ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake. Masimulizi yaliendelea kupamba moto huku wengine wakijisahau kama kuna kulala.


********

Asubuhi iliwasili kwa mbwembwe huku majogoo yakihitimisha majukumu yao ya kuwaamsha watu kama ilivyo ada. Viongozi walituamsha tukafanye usafi wa mazingira kwa maeneo yetu ya kila siku kwa kutukumbusha kuwa, tuwe waangalifu katika kukusanya mabaki ya salama soksi yaliyoonekana kuzagaa kila kona kabla jua halijachomoza. Tulifanya usafi kwa kiwango maridhawa kwa lengo la kuificha aibu iliyotendeka usiku kucha. Mnamo saa moja kamili za asubuhi kengele iligongwa kutukutanisha na wageni wetu ili kufanya tathimini ya sherehe na pia kwa kutambulishana na kuagana. Alianza kusimama matroni kutoka Kibondo na kuanza kusema “Ndugu walimu, walezi na wanafunzi kwa ujumla, sina maneno mengi zaidi ya shukrani za upendo wa dhati kutoka kwenu, mmetufanyia mambo mengi na mazuri kuliko miaka yote iliyopita na kwa mwaka huu ninasema imekuwa kufuru. Amani imechukua nafasi kubwa ingawa kuna dosari ndogo ndogo zilizojitokeza hasa kwa upande wangu kuna binti mmoja niliyekuja naye aitwaye Shamia alipatwa na tatizo ingiwa si kubwa sana. Huyu alikatwa ngwara au mtama na kijana mmoja asiyefahamika baada ya kukataa kucheza naye muziki. Binafsi nasema huo ni ushamba na ulimbukeni kwa wasomi kama nyie msiofahamu kuwa, chakulazimishana mara nyingi huwa hakinogi.” “Naimani kuwa hakuna mambo mabaya yaliyofanyika kama tulivyowaasa.” Alipofikia hapo wanafunzi wote waliitikia kwa pamoja kwa sauti kuu, “Ndiyo mamaaa!” Matroni akaendelea, “Kama kuna uchafu uliofanyika kwa uficho, mjue kuwa hapa duniani hakuna siri iliyowahi kufichika kwani hata kuitishwa kwa mkutano wa Berlin wa mwaka 1884 – 1885 ilisadikika kuwa ni siri lakini wajumbe walienda wakiwa na ukweli mikononi kuwa lengo ni kuligawa bara la giza. Hivyo na mimi ninasema, kama ulifanya upuuzi wowote gizani ipo siku utakuwa mwangani na wahusika kubakia na aibu kubwa kwani waswahili husema, “Mjichambia jani bichi la mgomba huondoka na mbolea yake makalioni.” Matroni huyo alihitimisha. Kwa upande wa mwalimu mwenyeji, yeye hakusema mengi zaidi ya kuwatakia safari njema wageni wetu. 


********

Tulipewa muda wa kupeana majina ya utambulisho na anuani za makazi kwa minajili ya kudumisha urafiki kwa njia ya mawasiliano ya barua. Tulibadilishana anuani kwa kuziandika kwenye shajara zetu huku tukipongezana kwa shughuli pevu ya jana yake. Tulielekea kwenye kifungua kinywa ili tuwape wenzetu wasaa wa kujiandaa kwa safari ya kuelekea Kibondo. Mnamo saa tatu asubuhi tulikusanyika kwenye gari aina ya Isuzu kwa lengo la kuagana na wageni wetu. Tuliagana kwa mtindo wa kukumbatiana huku tukimwagiana mabusu ya mficho mficho kwani siku zote la ubaya halina mwanga. Katika maagano yetu nilikumbana na mkumbatio wa vifua tofauti tofauti vyenye msisimuo ulioshtua hisia zangu kwa mara nyingine. Aliyeniacha hoi ni Latipha, Yule dada aliyemchamba Shamia usiku ule ndani ya ukumbi wa disko. Yeye alinikumbatia huku mkono wake mmoja akiukosesha adabu kwa kuupeleka kwenye chururu yangu bila hata aibu huku wenzake waliotuzunguka wakimtazama kwa macho ya kumwambia, “Uyafanyayo hayafanywi hadharani.” Latipha hakuwajali bali aliendelea na utundu wake huo ambao ulinifanya niwe kama sanamu iliyosimamishwa kwa minajili ya maonesho. Alinilamba lamba eneo la sikio langu huku akininong’oneza kwa maneno haya, “Jana uliamua kunibania kwa kutokuja kwenye disko lakini nakuapia kuwa, nitakutafuta popote utakapokuwa wakati wa likizo ili niifanikishe adhima ya moyo wangu. Tumeumbwa ili tupeane vya bayana na tafsida ila wewe unajifanya kuwa mgumu. Ulikabidhiwa hiyo chururu yako kwa malengo ya kuchurururisha zaidi ya mkojo ila wewe hautaki kuitimizia haja yake muhimu hapa duniani, hebu yatimize malengo hayo usije ukafukiwa nayo ikawa zaidi ya mchwa na mafunza.” Aliniachia kwa busu ambalo nilihisi kuwa ngoma ya sikio langu imepasuka. Hayo ni miongoni mwa mabusu ambayo hubusiwa watu wenye nyota za kupendwa na hawa viumbe wa kike kama kina sisi.

====>>Itaendelea wiki ijayo...


Usiikose SEHEMU YA 12>>> ya Riwaya hii ifikapo Jumatatu ya wiki ijayo, na utaipata hapa Zero Degree pekee.
Fumanizi la Mapenzi: Sehemu ya 11 Fumanizi la Mapenzi: Sehemu ya 11 Reviewed by Zero Degree on 7/07/2017 12:23:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.