Loading...

Rooney alivyoiongoza Everton kuichapa Gor Mahia goli 2-1


Mshambuliaji Wayne Rooney amefanya kile walichotaka kuona mashabiki wa soka Tanzania baada ya kuiongoza Everton kuichapa Gor Mahia kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Rooney alifunga bao la kwanza kwa Everton kwa shuti la umbali wa mita 30 akimtungua kipa wa Gor Mahia, Boniface Oluoch katika dakika 34.

Bao la Rooney limefanya aweke rekodi mpya katika klabu hiyo kwani mwaka 2002 akiingia akitokea benchi katika mechi ya Ligi Kuu dhidi Arsenal alifunga bao lake kwa shuti la umbali wa mita 25, linalofanana na hili la leo Alhamisi Julai 13, 2017 dhidi ya Gor Mahia.

Bao hilo la Rooney lilidumu dakika nne kwani dakika 38, Gor Mahia ilisawazisha bao hilo kupitia kwa Tuyisenge akiuunganisha kwa kichwa krosi na kuzifanya timu hizo kwenda mapumziko matokeo yakiwa bao 1-1.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote mbili kufanya mabadiliko ya wachezaji wake, lakini ni Everton iliyofaidika zaidi katika na mabadiliko hayo.

Everton ilitawala sehemu kubwa ya kipindi hicho na kufanya mashambulizi ya mara kwa mara langoni kwa Gor Mahia.

Wakati mashabiki wakiamini mechi hiyo itamalizika kwa sare, kiungo Kieran Dowell alipokea mpira akiwa nje kidogo ya eneo la 18, alipiga shuti lililokwenda moja kwa moja wavuni katika dakika 81.

Ushindi huo ni mwanzo mzuri kwa Everton inayojiandaa na mechi ya kusaka kufuzu kwa Europa Ligi mwanzoni mwa mwezi ujao.
Rooney alivyoiongoza Everton kuichapa Gor Mahia goli 2-1 Rooney alivyoiongoza Everton kuichapa Gor Mahia goli 2-1 Reviewed by Zero Degree on 7/14/2017 01:02:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.