Loading...

Video: Real Madrid yakubali kichapo cha goli 4-1 kutoka kwa Manchester City


Klabu ya Manchester City imechomoza na ushindi wa mabao 4 – 1 dhidi ya Mabingwa wa klabu bingwa barani Ulaya Real Madrid mchezo uliyochezwa jana alfajiri.

Nicolas Otamendi ndiye aliyeanza kuipatia City bao la kwanza katika dakika ya 52, kisha Raheem Sterling akiifungia bao la pili dakika ya 59 na latatu likifungwa na John Stones katika dakika ya 66 ya mchezo huo kisha Brahim Diaz akimalizia karamu ya magoli manne kwa City katika dakika ya 81 akiwa anatokea benchi.

Wakati bao la Madrid likifungwa na mchezaji, Arnaiz Oscar katika dakika za lalakwa buriani 90, akiwa umbali wa mita 30 kutoka eneo alilokuwepo kipa wa City na hivyo kuwa bao bora katika mchezo huo wa International Champions Cup uliyochezwa Los Angeles nchini Marekani leo. Katika mchezo huo mchezaji,Kevin De Bruyne ndiye aliyechaguliwa kuwa mchezaji bora.

Sasa Manchester City inatarajia kuwakabili Tottenham Julai 29 huko Tennessee kabla ya kumaliza maandalizi yao ya msimu mpya wa ligi dhidi ya West Ham huko Iceland Agosti 4 mwaka huu.

Video: Real Madrid yakubali kichapo cha goli 4-1 kutoka kwa Manchester City Video: Real Madrid yakubali kichapo cha goli 4-1 kutoka kwa Manchester City Reviewed by Zero Degree on 7/27/2017 05:00:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.