Loading...

Tundu Lissu ameachiwa kwa dhamana


Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) na Mbunge wa Singida Mashariki kupitia tiketi ya CHADEMA, Mhe. Tundu Lissu ameachiwa kwa dhamana ya Milioni 10 leo katika kesi yake iliyokuwa inamkabili ya uchochezi.

Mahakama ya Kisutu imempa dhamana Mhe Tundu Lissu kwa sharti la kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini dhamana yenye thamani ya Shilingi milioni kumi, uamuzi uliotolewa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu, Wilbard Mashauri.

Mhe Lissu alikuwa anatetewa na jopo la mawakali 18 likiongozwa na Fatma Karume na Peter Kibatala ambapo katika shauri la kwanza waliomba Mahakama impe dhamana mteja wao.

Mwanasheria huyo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA alitiwa nguvuni mnamo Julai 20 siku ya alhamisi katika uwanja wa ndegewa Mwl Nyerere akiwa anaelekea nchini Rwanda.
Tundu Lissu ameachiwa kwa dhamana Tundu Lissu ameachiwa kwa dhamana Reviewed by Zero Degree on 7/27/2017 05:21:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.