Loading...

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza ulinzi uimarishwe mipakani


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Tanzania siyo lango la kupitishia dawa za kulevya kwenda nchi za nje hivyo ameagiza ulinzi uimarishwe katika mipaka yote.

Mh. Majaliwa alitoa kauli hiyo jana jioni, Julai 29, 2017 alipozungumza na watumishi wa kituo cha forodha cha Kasumulu kilicho katika mpaka wa Tanzania na Malawi wilayani Kyela na kusema jambo hilo linatakiwa kudhibitiwa na kusema kwamba ni vyema ukaguzi wa watu wanaopita kwenye maeneo hayo pamoja na mizigo ukaimarishwa.

“Endeleeni kufanya upekuzi wa kina wa magari, watu na mizigo yote yote katika mipaka yetu. Tanzania siyo lango la kupitishia dawa za kulevya na Serikali haitakubaliana na jambo hilo.”

Pia aliwataka viongozi hao kuhakikisha biashara zote za magendo zinazifanyika mipakani, zikiwemo za kubadilisha fedha zinadhibitiwa kwa kuwa zinaikosesha Serikali mapato.

Alisema ni vema yakawepo maduka ya kubadilishia fedha katika maeneo hayo ili kudhibiti biashara hiyo ambayo kwa sasa inafanywa kimagendo huku Serikali ikikosa kodi.

“Biashara za magendo zidhibitiwe katika maeneo haya na yaanzishwe maduka ya kubadilishia fedha ili biashara hiyo ifanyike kihalali. Pia imarisheni vyanzo vya mapato," aliongeza.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza ulinzi uimarishwe mipakani Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza ulinzi uimarishwe mipakani Reviewed by Zero Degree on 7/30/2017 07:55:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.