Loading...

China yamtaka Rais Donald Trump kuchunga matamshi yake


Rais wa China Xijinping amemtaka rais Donald Trump kuchunga mtamshi na vitendo vinavyozidisha hali ya kuzua wasiwasi, chombo cha habari cha kiserikali kimeripoti.

Rais Trump na Korea Kaskazini wamekuwa wakirushiana cheche za maneno huku rais huyo wa Marekani akionya kuikabili kivita Korea Kaskazini.

Lakini China ambaye ni mshirika mkuu wa Korea Kaskazini ametaka pande zote mbili kuwa na uvumilivu.

Taarifa ya ikulu ya Whitehouse imesema kuwa Marekani na China zilikubaliana kwamba Korea Kaskazini inafaa kusitisha uchokozi na tabia mbaya.

Hofu kubwa inayoendelea kutanda kuhusu mpango wa kinyuklia wa Korea Kaskazini ilizidi baada ya taifa hilo kufanyia majaribio makombora yake ya masafa marefu mnamo mwezi Julai.
China yamtaka Rais Donald Trump kuchunga matamshi yake China yamtaka Rais Donald Trump kuchunga matamshi yake Reviewed by Zero Degree on 8/12/2017 01:38:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.