Coutinho atuma maombi ya uhamisho baada ya Barcelona kutangaza dau
Siku ya leo Ijumaa asubuhi, 'Fenway Sports Group' imetoa taarifa inayodai kwamba, hakuna ofa yoyote itakayopokelewa kwa ajili ya kumsajili Coutinho katika majira haya ya joto, na kocha Jurgen Klopp akishikiria msimamo wa bosi wake.
Ripoti ya klabu ilisomeka hivi: "Klabu haitakubali ofa yoyote itakayotolewa kwa ajili ya kumsajili Philippe na atabakia kuwa mmoja wa wanafamilia wa klabu ya ya Liverpool hadi kufungwa kwa dirisha la usajili katika majira haya ya joto."
Mtandao wa 'Sky Sports' unadai kwamba Liverpool tayari wamekataa ofa mbili zilizowekwa mezani na klabu ya barcelona pamoja na ile ya mwishoni iliyokadiliwa kuwa karibuni sawa na paundi milioni 90.4.
Hata hivyo, inaeleweka kwamba Barcelona wako tayari kulipa hadi paundi milioni 110 kwa ajili ya kumnsa Coutinho, ambaye alionyesha mapenzi na klabu yake ya Liverpool kwa kusaini mkataba wa miaka mitano na nusu mwezi Januari.
Hata hivyo, inaeleweka kwamba Barcelona wako tayari kulipa hadi paundi milioni 110 kwa ajili ya kumnsa Coutinho, ambaye alionyesha mapenzi na klabu yake ya Liverpool kwa kusaini mkataba wa miaka mitano na nusu mwezi Januari.
Meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp anasema kwamba, nafasi ya Coutinho ndani ya klabu inaeleweka hadi hivi sasa baada ya kauli iliyotolewa na bosi wa klabu jiyo kwamba hatauzwa.
"Wakati bosi anapoamua jambo flani, ni asilimia 100 kwamba mjadara umefungwa rasmi," alisema Klopp. "Unaweza ukajisomea kuhusu uamuzi huo wewe mwenyewe, sidhani kama kuna kipya cha kuongeza kuhusiana na hilo."
Klopp alithibitisha kuwa Coutinho ataukosa mchezo kati ya Liverpool na Watford kwa sababu ya majeraha aliyopata hivi karibuni na kuna hatari ya kuukosa mchezo wa kwanza wa kutafuta tiketi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa dhidi ya Hoffenheim katikati ya wiki.
Coutinho atuma maombi ya uhamisho baada ya Barcelona kutangaza dau
Reviewed by Zero Degree
on
8/11/2017 03:32:00 PM
Rating: