Loading...

Serikali yataifisha magari yaliyokutwa na Rais Magufuli bandarini

Mkurugenzi wa Mashtaka nchini, Biswalo Mganga
Serikali imetaifaisha magari matatu ya kifahari kati ya saba yaliyokutwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwenye makontena, alipofanya ziara ya kushtukiza bandarini na kubainika hayakuwa na Nyaraka stahiki.

Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Biswalo Mganga amesema kuwa Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu imeamuru washtakiwa wa magari hayo Sulatani Ibrahimu rai wa Uganda na Ramadhani Ukwaju wa Tanzania kulipa faini.

Kati ya Makosa wanaoyoshatikiwa nayo watuhumiwa hao ni pamoja na udanganyifu kwa maafisa forodha kuhusu vitu walivyokuwa wameviingiza nchini ambapo nyaraka zao walionyesha walikuwa wameingiza viatu na nguo za mitumba lakini kwenye makontena kulikua na magari hayo ya kifahari.

Aidha Kosa lingine wanaloshatikiwa watuhumiwa hao ni pamoja na kuisabiashia serikali hasaara ya zaidi ya milioni tisini kutokana kukwepa kodi lliyotokana na uingizaji wa magari hayo ya thamani kwa kulipa ushuru kidogo wa nguo na viatu.
Serikali yataifisha magari yaliyokutwa na Rais Magufuli bandarini Serikali yataifisha magari yaliyokutwa na Rais Magufuli bandarini Reviewed by Zero Degree on 8/11/2017 02:41:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.