Loading...

Tanzania yashuka nafasi 6 katika viwango vya FIFA


SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (Fifa), jana Alhamisi lilitoa viwango vya soka vya mwezi Julai kwa mataifa mbalimbali ambapo Tanzania imeshuka kwa nafasi sita kutoka 114 ya hadi 120.

Sehemu ya orodha hiyo iliyotolewa na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA)
Wakati kimataifa Tanzania ikishika nafasi ya 120, kwa upande wa Afrika ipo nafasi ya 35, huku ikiwa ya nne katika Ukanda wa Afrika Mashariki ambapo Uganda inaongoza ikifuatiwa na Kenya, kisha Rwanda na Burundi inaburuza mkia. Katika nafasi kumi za juu kwenye orodha hiyo, Brazil inaongoza ikifuatiwa na Ujerumani, Argentina, Uswizi, Poland, Ureno, Chile, Colombia, Ubelgiji na Ufaransa inahitimisha.
Tanzania yashuka nafasi 6 katika viwango vya FIFA Tanzania yashuka nafasi 6 katika viwango vya FIFA Reviewed by Zero Degree on 8/11/2017 02:33:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.