Kichuya kutimkia Uarabuni.!?
Tetesi za taarifa hizo ambazo zinahusu Kichuya kuondoka ndani ya Klabu ya Simba bado ziko uvunguni sana kwa madai kuwa Waarabu hawajafikia dau linalotakiwa ili kumtoa kiungo huyo machachari awapo uwanjani.
Pamoja na hayo, Manara anadaiwa kugoma kuweka wazi ni kiasi gani wanakihitaji kwa Kichuya na pia kukataa kuthibitisha ni timu ipi ya Misri ambayo imeshatangaza dau ndani ya klabu hiyo.
Kama uhamisho wa Kichuya ukikamilika kwenda Misri ni faida kubwa kwa Taifa kwa kuanza kuchezesha wachezaji wengi nje na kuleta soka lenye ushindani.
"Kichuya kuwavutia wamisri tunalifahamu, hata hizo tetesi za kuhusu kuondoka siwezi kuzithibitisha kwani dili halijakafika mezani. Lakini pia hao Waarabu wakija na mzigo wa kutosha ambao Simba tunauhitaji tutawapatia Kichuya lakini mpaka sasa nachoweza kusema bado Kichuya ni mali ya Simba SC", alisema Msemaji wa Simba Haji Manara wakati akifanya mahojiano na ukurasa huu.
Pamoja na hayo, Manara anadaiwa kugoma kuweka wazi ni kiasi gani wanakihitaji kwa Kichuya na pia kukataa kuthibitisha ni timu ipi ya Misri ambayo imeshatangaza dau ndani ya klabu hiyo.
Kama uhamisho wa Kichuya ukikamilika kwenda Misri ni faida kubwa kwa Taifa kwa kuanza kuchezesha wachezaji wengi nje na kuleta soka lenye ushindani.
Kichuya kutimkia Uarabuni.!?
Reviewed by Zero Degree
on
8/11/2017 02:18:00 PM
Rating: