Loading...

Kesi ya aliyekuwa rais wa TFF, Jamal Malinzi na wenzake yapigwa kalenda

Picha ya mtandao
UPANDE wa utetezi katika kesi inayomkabili aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Sola nchini (TFF), Jamal Malinzi na wenzake, umeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutoa maelekezo mahsusi kwa upande serikali kuharakisha upelelezi dhidi ya washitakiwa, kinyume na hapo mahakama iwasikilize na iwaachie huru.

Akiieleza mahakama hiyo, wakili wa utetezi, Domician Rwegoshora, amemweleza Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, kwamba wanautaka upande wa mashtaka uharakishe upelelezi kwa sababu kesi hiyo haina dhamana, hivyo washtakiwa wakiendelea kukaa ndani wanateseka.

”Naiomba mahakama itoe maelezo mahsusi kwa upande wa mashtaka kwa muda mfupi, au washtakiwa wasikilizwe ikiwezekana mahakama iwaachie,” alisema Domician.

Baada ya kueleza hayo, Wakili wa Serikali, Vitalis Peter, akasema kuwa upelelezi upo katika hatua ya mwisho na muda si mrefu kesi itaanza kusikilizwa.

Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi Septemba 9, mwaka huku akiutaka upande wa serikali kuharakisha na ikiwezekana katika tarehe hiyo watoe taarifa kuhusu upelelezi ulipofikia.
Kesi ya aliyekuwa rais wa TFF, Jamal Malinzi na wenzake yapigwa kalenda Kesi ya aliyekuwa rais wa TFF, Jamal Malinzi na wenzake yapigwa kalenda Reviewed by Zero Degree on 8/24/2017 02:46:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.