Loading...

SportPesa yazindua Promosheni ya 'Rafiki Bonasi'

Mkurugenzi Mkuu SportPesa, Pavel Slavkov
KAMPUNI ya SportPesa imezindua rasmi promosheni ya mtambulishe rafiki ijulikanayo kama "Rafiki Bonus" ambapo mtambulishaji atajipatia Sh. 2000/- kama 'bonasi' ya utambulishaji huo.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa juzi na Mkurugenzi Mkuu SportPesa, Pavel Slavkov, alieleza kuwa mteja wa SportPesa ambaye tayari ameshajisajili na kuanza kucheza, anachotakiwa kufanya ni kumtambulisha rafiki yake ambaye akijisajili na akianza kucheza, aliyemtambulisha atapata bonasi ya Sh. 2000/-.

“Kampuni imekuja na "Bonus ya Rafiki" ikiwa kama njia ya kurudisha fadhila kwa wateja wetu. Tunawafurahia wateja wetu, na tunajua kuwa wamekuwa wakiwafundisha rafiki zao namna ya kubashiri na SportPesa. Hivyo basi, tumeona ni vyema na sisi tuwawekee mazingira ya wao kunufaika kwa uaminifu wao na Kampuni. 

"Bonus ya Rafiki inamuwezesha mteja kupata Sh. 2,000, kwa kila mteja anayemtambulisha katika jukwaa la kubashiri na SportPesa,” alinukuliwa Slavkov katika taarifa hiyo. 

Alisema, ili mteja aweze kufuzu kushiriki katika bonasi ya Rafiki; mteja anatakiwa awe amejisajili na awe mtumiaji wa SportPesa kubashiri.

Pia, mteja mpya ambaye anatambulishwa na rafiki yake, anatakiwa kutuma neno KUBALI kisha kuandika namba ya simu ya mtu aliyemkaribisha katika jukwaa la kubashiri la SportPesa, mfano KUBALI 0700XXXXXX.

Mteja mpya atatakiwa kuweka ubashiri angalau mara moja katika michezo ya Jackpot, kwenye mchanganyiko wowote wa Multi Bet bila kujali aina ya mchezo, au kuweka 'Single Bet' kwenye mechi yoyote ya mpira wa miguu yenye soko la njia tatu (1,X,2) - yaani ushindi wa nyumbani (1), suluhu (x) au ushindi wa ugenini (2) ambapo 'odds' za soko atakalochagua ziwe zaidi ya 1.60.

"Mteja anaweza kubashiri kwa njia ya ujumbe (SMS) au kwa njia ya tovuti (www.sportpesa.co.tz) ambapo atafuata hatua zilizoelekezwa, ili kushiriki kwenye bonasi hiyo. 

Uzinduzi wa "Rafiki Bonus" ni sehemu moja wapo ya Kampuni ya SportPesa katika kuwaburudisha wateja wake ambao, kwa kipindi kirefu sasa tangu kuanza shughuli zake nchini, wamejisajili kikamilifu na wengi wao wamesaidia rafiki, ndugu na jamaa kujiunga na kubashiri kutumia majukwaa ya Sportpesa," alisema. 

SportPesa inajivunia kuwa na kiasi kikubwa cha pesa ya Jackpot kwa sasa, cha fedha za Kitanzania milioni mia mbili na tatu (Sh. 203,391,920), 'odds' zinazovutia na huduma kwa wateja yenye daraja la kimataifa iliyopo hewani saa 24 kuwafikia wateja waliopo na wapya wanaopenda kujua zaidi kuhusu huduma za kampuni.

Wateja wanashauriwa kupiga simu za huduma kwa wateja 0764 115 588, 0658 115 588 na 0692 115 588 kwa taarifa zaidi kuhusu bonasi ya rafiki.
SportPesa yazindua Promosheni ya 'Rafiki Bonasi' SportPesa yazindua Promosheni ya 'Rafiki Bonasi' Reviewed by Zero Degree on 8/11/2017 01:21:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.