Loading...

Fumanizi la Mapenzi: Sehemu ya 21



MTUNZI: MC Short Charles Gwimo

Ilipoishia.........Madam na mwalimu Kishoto waliagana kwa mabusu ya kinafiki huku nikiujua ukweli wa upande mmoja na kusahau kuwa, “Kilichompata ngwena na kiboko ndicho.” Waliagana kwa mashamsham kwa kurushiana mabusu ya hewani huku madam akuizidisha uongo kwa kumwambia, “Ningekufikisha mbali ila tu pedi sijaibana vizuri. Tutaonana eeh!”

Endelea nayo: Kuondoka kwa mwalimu Kishoto mle ofisini kulinifanya nipumue kwa Amani nikiamini kuwa nimekwepa fumanizi la mchana la kufumaniwa na mwalimu aliyesifika kwa uchapaji wa viboko hasa pale linapotokea suala la kimaadili. Nilijitoa mle kwenye chumba cha huduma ya kwanza na kuja kukaa kwenye ofisi ya madam ambaye alikuwa bado yuko nje akiyatafakari mambo mawili kwa mpigo ambayo ni penzi changa kutoka kwangu na maneno ya huba kutoka kwa mwalimu kishoto. Nilikaa kwenye kiti cha madam kana kwamba mimi ndiye huku nikijifanya kupanga panga vitu vizuri mithili ya mfanyakazi aliyemaliza kazi zake salama hivyo yuko anataka kufunga ofisi ili aelekee nyumbani kwa minajili ya kujipumzisha. Niliendelea kuvipanga panga vitu hivyo mpaka pale nilipokutana na kitabu kimoja cha simulizi za kimapenzi kilichoandikwa “MAPENZI NDANI YA TRENI”. Nilikipitia juu juu kwa kukitazama picha tu ili madam asinifume kwenye miongoni mwa vitabu vyake vya siri. Nilivutiwa na picha mbalimbali zikiwa zimechorwa kwa mtindo wa matamanio kwa wanaume wote wenye kusisimkwa na viuno vyao vya uzalishaji jamii. Kwa kuwa nilikuwa na begi langu la madatari, moyo ulinisukuma nikiibe kijarida hicho lakini mawazo mengine yakanionya nisithubutu.

**********

Madam alirudi ofisini na kunikuta niko juu ya kiti chake pasina hata chembe ya uoga kama nilivyokuwa hapo awali wakati naingizwa ofisini humo. Nilimkaribisha madam kama vile mwalimu ampokeavyo mgeni maalum ofisini. Madam aliachia tabasamu zito la kunikubali huku akiuachia mwanya wake wa chini ulionogeshewa kwa meno meupe kama theluji kinywani mwake. Alinisogelea nilipokuwa nimekaa kisha akanipiga busu la kinywa kwa kinywa kisha akaanza kunisifu kwa sifa za nyongeza “Hakika Devi, wewe ni mtoto wa kiume uliyetunukiwa sifa zote za uanaume, kwa umri wako huo mdogo umeweza kunifikisha mwisho wa safari na bado nataka kusafiri. Je siku ukiwa mtu mzima ndani ya safari kwa gari lako mwenyewe ni nani atayekwepa kupandishwa kwenye gari lako?” Nilimjibu kishababi, “Madam, haya mambo ndiyo kwanza napatia uzoefu kwako. Hivyo basi, naamini kama utaendelea kuniweka kwenye ratiba zako za kila siku na mimi nitakuwa dereva mwenye uzoefu kwenye fani hii takatifu.” Niliendelea, “Madam, najua unifikiriavyo sivyo nikuwazavyo, binafsi nimeshajitoa kuwa mtumwa wa mapenzi kwako kwani naamini hakuna mwingine atakayekuwa mtamu zaidi yako hata kama kina mwalimu Kishoto watajiwekea makazi ya kudumu kwako, mimi nitakuwa mkia wa mbuzi kwenu.”


**********

Niliendelea kumsogesha madam kwa soga zenye vina vya kimapenzi kama vile mshauri nasaha anatoa dozi ya nasaha kwa mwanadada aliyepigwa kibuti na mwenzi wake. Niliyapanga maneno kama nilivyofundwa na rafiki yangu kipenzi Mood aliyewahi kunisimulia ya kwamba, hakuna mwanamke anayekubali ukweli wowote kutoka kwa mwanaume zaidi ya kuamini uongo kwa asilimia zote. Madam Linda aliniamini kwa yote niliyomuelezea nikijinadi kwake kuwa yeye ndiye wa kwanza kuniingiza kwenye dimbwi la huba huku shajara yangu ya mapenzi moyoni ikiwa na majina ya Shamia na Fauzia tulioendana kwa rika. Siku hiyo madam hakupenda kunipa nafasi ya kuelekea bwenini kuungana na wenzangu ukizingatia tulikuwa kwenye maandalizi ya kuandika mitihani ya kumaliza muhula wa kwanza wa masomo.


**********

Madam aliniacha ofisini kwake kisha akatokomea sehemu ambayo sikuitambua. Aliporudi alikuja amebebelea mifuko miwili ya kaki iliyokuwa imesheheneshwa chips mayai na kuku wa kukaangwa. Alinikabidhi mfuko mmoja naye mwingine kisha tukaanza kujilia vyetu. Madam akiwa amenogewa kwa penzi langu hakusita kunisifia huku akiwalaani wazazi wangu kwa kuchelewa kunizaa. “Devi, mpenzi ulivyomtamu kwa umri huo mdogo, Je, ukisogea zaidi ya hapo, kina dada si tutakupangia foleni kama magari ya barabara za bongo?” “Tena Devi wangu, binasi nawalaumu wakwe zangu kwa kuchelewa kukuleta duniani ilihali kina Linda, tulikuwa tunakusubiri kwa hamu.” Nilijichekea moyoni huku nikiitengeneza taswira ya pesa kichwani mwangu nitakazokuwa napewa kwa ajili ya matumizi yangu kama madam alivyoniahidi. Nilimuwazia sana mwalimu Kishoto jinsi atakavyochunwa pesa yake na mimi kumsaidia madam kuzitafuna.


**********

Nilitafuna chips zangu zote kwa mtindo wa kufakamia kwani msosi kama huo ulikuwa ni sawa na kukuokota dodo chini ya mkuyu. Ndugu msomaji wangu, kwenye mapenzi hata ujinga husifiwa. Kwa kitendo cha kufakamia msosi kwa mtindo ule halafu madam anaanza kunisifia eti mimi ni dume la shupaza kwenye mchezo wa karata. Kwa upande wangu nilijisikia vibaya kwa kusifiwa sifa kinyume badala ya kuitwa mlafi au mlaku. Madam aliendelea kunipa vihadithi vingi vya kimapenzi na jinsi ya kufurahishana kwenye tendo la ndoa. Sikupenda kumuhoji eti hayo yote aliyajulia wapi kwani wahenga walisema “Akutangaye na jua hujua mengi.” Licha ya kuwa ni mwalimu wa somo la sayansi, Madam Linda alikuwa ni mfuatiliaji wa simulizi za mapenzi kama zile nilizokujuza za “Kibabu Changu” na “Mapenzi ndani ya treni.”


**********

Nilimuomba ruhusa madam aniruhusu nikaungane na wenzangu kwenye foleni ya chakula cha jioni ambacho huku kwetu hujulikana kama chakula cha usiku. Madam alisimama akaichukua pochi yake iliyokuwa inaonekana kama ina mjao wa neema ya mshiko. Alinichomolea noti kumi mpya mpya za shilingi miatano kwa ajili ya kunipa zawadi ya ushindi iliyokuwa inashindaniwa na wengi akiwemo mwalimu Kishoto. Nilizipokea noti zile za jero jero na kuzisunda kibindoni ili wenzangu wasijue kama ninamshiko na mkononi kubakia na PAJERO moja yaani shilingi miatano tu.


**********

Niliposema pajero najua msomaji wangu kidogo nikupoteza. Ukweli ni kwamba rejesta ‘jero’ ni kifupi cha pajero kwani kuingia kwa noti mpya za shilingi miatano kwa kipindi hicho cha miaka ya tisini na kuingia kwa magari mapya hapa Tanzania yenye nembo ya kibiashara iliyojulikana kama “PAJERO”...Ulizeni muambiwe ya wahenga ili muwajue wahenga kupitia misemo yao iliyopata athari za kimatamshi kwa kizazi cha utandawazi. Nilimuaga madam kwa kumshukuru kwa pesa aliyonipa ikiwa ni nyingi kuliko niliyotazamia. Licha ya kunipa pesa hizo pia alinipatia masazo ya chips kuku ili nikalishie msosi wa jioni.


**********

Nilimuaga madam kwa kumrushia busu la hewani ambalo naye alilirudisha kwa mtindo wa hewani. Nilitoka ofisini mwake nikiwa mwepesi kama vile kishada au tiara iliyoko hewani. Tabasamu halikubanduka usoni jambo ambalo kila mtu alitaka kujua ni kipi kilinipata kutoka kwa madam kwani waliomuona mwalimu Kishoto akizamia ndani mithili ya faru dume aliyejeruhiwa. Kwa kuogopa kuchukuliwa maelezo zaidi, niliwadanganya kuwa nimetubia madhambi yangu na kusamehewa. Nilijipenyeza hadi kwa rafiki yangu na kumpa moja ya masazo ya chips na kuku. Nilimuhadithia kila kitu isipokuwa lile la kulishwa tunda na madam. Sikumuweka bayana ili kumlindia heshima madam wangu aliyegekuaka kuwa mpenzi wangu.

====>>Itaendelea Jumatatu...

Usiikose SEHEMU YA 22>>> ya Riwaya hii ifikapo siku ya Jumatatu wiki ijayo, na utaipata hapa Zero Degree pekee.
Fumanizi la Mapenzi: Sehemu ya 21 Fumanizi la Mapenzi: Sehemu ya 21 Reviewed by Zero Degree on 8/11/2017 01:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.