Loading...

Video: Diego Costa awatupia Chelsea kombora jingine, Conte ajibu kwa ufupi


Diego Costa sasa ameituhumu Chelsea kuongeza ada yake ya uhamisho kukwamisha uhamisho wake kuelekea klabu yake ya zamani, Atletico Madrid.

Katika mahojiano aliyofanya na ESPN, Costa amesema kwamba kwa kiwango hicho kikubwa cha ada ya uhamisho walichoanza nacho Chelsea, ambacho kinakadiriwa kuwa paundi milioni 40 hadi 50 kitakwamisha mchakto mzima wa yeye kurejea Atletico Madrid katika majira haya ya joto.

“Nimejitathimini nakugundua mapenzi yangu yapo kwa Atletico pekee na nina hamu ya kuichea klabu yangu ya zamani, lakini kama Atletico na Chelsea hawatafikia makubaliano na Atletico wakishindwa kulitilia mkazo suala hili, siwezi kuendelea kuing'ang'ani klabu iyoonyesha kunipigani ipasavyo,” alisema Costa.

“Najua kwamba watatia juhudi, lakini kama ni kulipa kiasi ambacho Chelsea wanahitaji haitakuwa rahisi.

“Ninachojua ni kwamba, ofa hii ambayo Chelsea wanaitarajia itakuwa ni kubwa kuliko kiasi walicholipa wao (paundi milioni 32), hivyo nimewarudishia kila kitu kwa kila namna.”

Hata hivyo, Costa alikiri kutofahamu kiasi cha fedha halisi wanachokihitaji (Chelsea), lakini thamani yake imeathiriwa na kitendo cha Antonio Conte kumweleza bayana kwamba hatakuwa katika mipango yake kwa msimu huu.
“Sijui (kiasi cha fedha wanazohitaji), lakini wakala wangu alisema kwamba, Chelsea wanahitaji kiasi ambacho kitawafanya Atletico waachane na mimi,” aliongeza.

“Aliposikia kwamba Conte hakuwa na mipango na mimi tena, wakala wangu alielekea Atletico kujaribu kuzungumza nao kuona kama wananihitaji nirejee.


“Bila shaka, kwa maisha niliyoishi pale na yote niliyoyafanya pale, walionyesha kunihitaji tena, lakini hawatakuwa tayari kulipa kiasi kikubwa cha fedha. Atletico ni timu inayoendelea kukua kila mwaka, timu kubwa, lakini hawawezi kuvunja rekodi kwa kulipa kiasi kikubwa cha fedha.

“Wakati nilipojiunga na Chelsea walilipa kiasi kidogo cha fedha ukilinganisha na ofa ambayo wao wamepewa. Nafikiri wanatakiwa kufikiria ni kiasi gani na mimi nimewatendea. Sio mimi niliyesababisha suala langu kuwa nje ya klabu hadi sasa. Kama ingelikuwa ni matatizo yaliyosababishwa na mimi basi ningekuwa naichezea timu yangu hadi muda huu. Ni mwezi mzima sasa umepita na  rikizo kweli ni nzuri lakini zinachosha wakati mwingine.


“Sikuwa chanzo cha haya yote kutokea, lakini sasa imefika muda klabu itazamie mambo haya. Bila shaka wanahitaji kurudishiwa kitu [katika fikra za kisoka], kama vile kile nilichowapa pale nilipokuwa uwanjani, lakini pia suala la kifedha kwa ujumla. Baada ya miaka mitatu watapewa kiasi cha fedha zaidi ya kile walicholipa wao.”

Kwa upande wake Antoni Conte kuhusu suala Costa kuieleza 'Daily Mail' kwamba Chelsea inamchukulia kama mhalifu tangu alipotumiwa ujumbe kwa njia ya simu, alisema kwamba 
Costa amevuka mipaka kwa kusema hayo.

Alipoulizwa kuhusiana na hilo, Conte alishindwa kujizuia na kujikuta mwenye hali ya kukamatwa na kicheko juu ya hilo ambalo mhisipania huyo analichukulia kwa namna nyingine, kupitia taarifa ya 'Sky Sports':

Conte alisema, “Kila mmoja aliyekuwa Chelsea anajua ni nini kilitokea msimu uliopita” kabla ya kueleza kuwa muda wa Costa chini ya uongozi wake umekwisha tayari, alimalizia kwa kuongeza: “Alishapitwa na wakati. Achana na suala hilo kwa wakati huu.”

Tazama alichojibu Conte alipokuwa akihojiwa katika video hiyo hapo chini:
Video: Diego Costa awatupia Chelsea kombora jingine, Conte ajibu kwa ufupi Video: Diego Costa awatupia Chelsea kombora jingine, Conte ajibu kwa ufupi Reviewed by Zero Degree on 8/18/2017 08:28:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.