Loading...

Viwanda 10 vilivyobinafsishwa kwa wawekezaji vyarejeshwa serikalini


Serikali imerejesha kwenye miliki yake viwanda kumi vilivyobinafsishwa kwa wawekezaji na kushindwa kuendelezwa kwa mujibu wa mikataba ya makabidhiano huku ikitoa muda wa uangalizi kwa viwanda vingine 28 vinavyosuasua hadi kufikia tarehe 22 mwezi huu viwe vimeainisha mpango kazi wa uzalishaji unaoeleweka la sivyo na vyenyewe vitatwaliwa na kugawiwa kwa watu wengine wenye uwezo wa kuviendesha.

Waziri wa viwanda biashara na uwekezaji Mhe. Charles Mwijage amevitaja viwanda vilivyorejeshwa serikalini kuwa ni pamoja Mbao Mkata, Korosho Lindi, Chuma Taifa Manawa Ginnery, Tembo cheap board na Mangula mekanical tools, vingine ni mgodi wa Pugu dabaga tea factory, Polysacks DSM na kiwanda cha nguo Kilimanjaro kilichopo Arusha huku akisema orodha hiyo sio ya mwisho kwani bado zoezi hilo linaendelea.

Zoezi la kubaini viwanda hivyo limefanywa na kamati maalum chini ya msajili wa hazina kwa kushirikiana na serikali za mikoa wizara husika na wizara za kisekta na mwanasheria mkuu wa serikali ambapo waziri Mwijage anabainisha pamoja na kutaifishwa kwa viwanda hivyo vingine 11 vimeanza kufanya kazi kufuatia agizo la mhe rais john pombe magufuli alilolitoa la tarehe 22 june la kutaka viwanda vyote vianze uzalishaji.

Aidha waziri Mwijage amewataka wananchi kuthamini bidhaa zinazozalishwa na viwanda vya ndani ili viwe endelevu huku akiahidio serikali itahakikisha inaweka mazingira mazuri ya uwekezaji katika viwanda ili kuvutia wananchi wengi kuingia kwenye sekta hiyo.

Miaka ya nyuma serikali ilibinafsisha jumla ya viwanda 156 ambapo mpaka sasa viwanda vinavyofanya kazi ni 62 viwanda 28 vinasusua visivyofanyakazi kabisa 56 na viwanda 10 vikibinafsishwa kwa kuuzwa mali mojamoja.
Viwanda 10 vilivyobinafsishwa kwa wawekezaji vyarejeshwa serikalini Viwanda 10 vilivyobinafsishwa kwa wawekezaji vyarejeshwa serikalini Reviewed by Zero Degree on 8/11/2017 09:42:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.