Loading...

Chelsea waamua kuvunja mkataba wa mshambuliaji wao na kumwacha huru


Kwa mujibu wa ripoti za mitandao mbalimbali, Chelsea wameamua kumwacha mshambuliaji Loic Remy ajiunge na Las Palamas kama mchezaji huru baada ya kuuvunja mkataba wake.


Mshambulioaji huyo mwenye miaka 30 amekua akijitahidi kusaka nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza bila mafanikio tangu awasili Chelsea kutokea QPR kwa paundi milioni 10.5 miaka mitatu iliyopita.

Remy alikuwa Crystal Palace kwa mkopo msimu uliopita, lakini matumaini yake yalipotea baada ya kushindwa kuonyesha uwezo wake kufuatia kupata majeraha yaliyomfanya akae nje ya dimba kwa kipindi kirefu sana na kufanikiwa kucheza mechi nane pekee.

Baada ya kushindwa kumshawishi meneja Antonio Conte amuorodheshe kwenye kikosi chake katika michezo mitatu ya ufunguzi msimu huu wa 2017-18, ripoti zinadai kuwa Mfaransa huyo ameachwa huru na tayari amejiunga na Las Palmas ya Spain.

Klabu za Marseille, Everton, Swansea City na Newcastle United walikuwa wakihusishwa na kutaka kumsajili Loic Remy wakati wa dirisha dogo la usajili, lakini inadaiwa kuwa Las Palmas ndio waliofanikiwa kumsajili akiwa kama mchezaji huru.
Chelsea waamua kuvunja mkataba wa mshambuliaji wao na kumwacha huru Chelsea waamua kuvunja mkataba wa mshambuliaji wao na kumwacha huru Reviewed by Zero Degree on 9/02/2017 08:42:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.