Loading...

Chelsea imeingia kwenye kinyang'anyiro cha kusaka saini ya kiungo wa Brazil


Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na 'Daily Mail', Chelsea wameonyesha nia ya kutaka kumsajili kiungo wa klabu ya Gremio, Arthur Melo.

Meneja wa Chelsea, Antonio Conte anatazamia kuongeza nguvu katika safu ya kiungo kwenye kikosi chake, na Mbrazil huyo anaonekana kuwa ndiye chaguo lake la kwanza.

Arthur Melo
Chipukizi huyo (Arthur) ameonesha kiwango cha hali ya juu msimu huu, huku akionekana kuzivutia klabu nyingi kubwa barani ulaya na tayari ameitwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Brazil. Hata hivyo, bado hajalichezea taifa hilo hata mchezo mmoja.

Klabu za Manchester United, Barcelona na Atletico Madrid zote zimekuwa zikihusishwa na kiungo huyo, ambaye mfumo wake wa uchezaji umekuwa ukifananishwa na wa Andres Iniesta.

Manchester United wanahisi wana nafasi kubwa ya kumsajili Athur, lakini kwa upande mwingine, klabu ya Chelsea itakuwa na matumaini ya kumshawishi atue Stamford Bridge.

Chelsea wana wachezaji wengi wenye asili ya Brazil kama; Willian, David Luiz, Kenedy na Wallace ambao wanaweza kumshawishi Athur aichague klabu hiyo.
Chelsea imeingia kwenye kinyang'anyiro cha kusaka saini ya kiungo wa Brazil Chelsea imeingia kwenye kinyang'anyiro cha kusaka saini ya kiungo wa Brazil Reviewed by Zero Degree on 11/12/2017 12:02:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.