Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 12 Novemba, 2017

Mshambuliji wa Timu ya Taifa ya Ufaransa na Arsenal, Olivier Giroud
Olivier Giroud anasema kuwa hajutii uamuzi wake wa kusalia Arsenal baada ya kuifungia Ufaransa kwa mara nyingine tena.

Chris Coleman anadai Gareth Bale ataichezea Wales katika michuano ya 'China Cup' mwezi Machi mwakani kama hali yake itakuwa imeimarika.

Gareth McAuley anaweza kustaafu kucheza soka la kimataifa endapo meneja wa Timu ya Taifa ya Ireland, Michael O'Neill atajiuzulu. (Telegraph)

Manchester City watampa Raheem Sterling mkataba mpya baada ya kuanza msimu huu kwa kuonyesha kiwango cha hali ya juu.

Juventus wana mpango wa kumtumia Sami Khedira kumnasa nyota wa klabu ya Liverpool, Emre Can.

Kevin Mirallas
David Moyes atampa mkataba wa mwaka mmoja mchezaji wake wa zamani wa Everton, Kevin Mirallas katika klabu ya West Ham.

Real Madrid wametangaza dau lao la kwanza kwa anayetaka kumsajili Gareth Bale kuwa ni paundi milioni 85.

Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho ameshauriwa kumuuza Marouane Fellaini mwezi Januari kabla ya kufanya usajili wa wachezaji wapya.

Sam Allardyce
David Unsworth na Joe Royle wanatazamia kukumbana na hali ngumu endapo Sam Allardyce atachukua majukumu ndani ya klabu ya Everton.

Chelsea wanatarajiwa kufanya uteuzi wa atakayechukua nafasi iliyoachwa na Michael Emenalo mwisho wa msimu huu.

Philippe Coutinho amejiandaa kukabiliana na gadhabu ya meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp kwa kutangaza kuwa yuko tayari kuivaa Uingereza.

Fernando Torres atazamia kurejea Ligi Kuu ya Uingereza, akiziweka klabu za Newcastle na Southampton kwenye mstari wa mbele.

Mshambuliaji wa Newcastle, Aleksander Mitrovic ategemewa kufanya maamuzo magumu ya kutimkia China. (Mirror)

Nyota wa klabu ya Liverpool, Emre Can anatarajiwa kuitosa Juventus na kujiunga na Manchester City kama mchezaji huru mwakani.

Fraser Forster anaamini kwamba, aliyekuwa meneja wake wa zamani katika klabu ya Southampton, Ronald Koeman anaweza kuwa chaguo bora kwa Timu yake ya Taifa ya Uholanzi.

Rais wa klabu ya Real Madrid, Florentino Perez
Rais wa Real Madrid, Florentino Perez ameruhusu kuanza kwa mkakati wa kuwania saini ya Eden Hazard baada ya mazungumzo baina yake na klabu ya Chelsea kukwama.

Real Madrid waeandaa kiasi cha paundi milioni 200 kwa ajili ya kumnasa nyota wa klabu ya PSG, Neymar Jr mwishoni mwa msimu huu. (Star)

Mauricio Pochettino
Mauricio Pochettino atasababisha vita kubwa kati ya klabu ya Manchester United na Paris Saint-Germain mwishoni mwa msimu huu.

Meneja wa klabu ya West Ham, David Moyes anaumizi kichwa kutafuta namna ya kuwafanya mashabiki wa klabu hiyo wawe na imani naye.

Chelsea wanakutana na hali ngumu kumbakisha Eden Hazard baada ya meneja wa Real Madrid, Zinedine Zidane kumfanya Mbelgiji huyo kuwa chaguo lake la kwanza kwenye majira ya joto mwakani. (Express)

Javier Hernandez
David Moyes amemhakikishia Javier Hernandez kwamba ana nafasi ya kufanya vizuri akiwa na West Ham.

Meneja wa Timu ya Taifa ya Uingereza, Gareth Southgate anasema kwamba, atakayekuwa mrithi wa nafai yake atafaidika sana mpango wa sasa wake wa sasa wa kukuza vipaji vya wachezaji chipukizi. (Observer)
Klabu za Manchester United, Manchester City na Tottenham Hotspur zote zilijaribu kumsajili, Jurgen Klopp kipindi alipokuwa na Borussia Dortmund.

Michael O'Neill
Meneja wa Ireland, Michael O'Neill ndiye anayeongoza katika kinyang'anyiro cha kuwania nafasi ya meneja wa Scotland, Gordon Strachan.

Everton na Leicester wanfanya mchakato wa kumsajili mshambuliaji wa New York City, Jack Harrison mwenye thamani ya paundi milioni 6 baada ya kuonyesha kiwango cha kuvutia. (Daily Mail)

Arsenal wanapanga kumsajili Wilfried Zaha kwa paundi milioni 35 kuziba nafasi ya Alexis Sanchez.

Klabu ya West Ham inamtaka Danny Ings kwa mkopo mwezi Januari, David Moyes akitazamia kumaliza mchakato wa kumfuatilia mshambuliaji huyo wa Liverpool.

Mshambuliaji wa Manchester City, Gabriel Jesus anadai bado hana uhakika wa kupata nafasi kwenye kikosi cha Brazil kitakachoshiriki kombe la Dunia mwaka 2018. (Sun)

Luis Campos
klabu ya Chelsea inafanya mipango ya kumnasa Luis Campos, ambaye anadaiwa kuwa na ujuzi mkubwa barani Ulaya aje kuziba pengo lililoachwa na mkurugenzi wao wa michezo, Michael Emenalo. (Times
Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 12 Novemba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 12 Novemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 11/12/2017 03:04:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.