Loading...

Wizara ya ujenzi yapewa mtihani mzito


RAIS John Magufuli ameiagiza Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kutafuta fedha na kujenga barabara ya Mutukula – Minziro yenye urefu wa kilometa 6 ili kurahisisha usafiri wa watu na mizigo.

Alitoa agizo hilo jana katika Mji wa Mutukula mpakani mwa Tanzania na Uganda baada ya kupokea kero za wananchi waliokusanyika jirani na geti la kuvuka mpaka huo ambao wamedai kukosekana kwa barabara hiyo kunawalazimu kutumia barabara ya kuzunguka Kyaka.

Pamoja na kumtaka Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kujenga barabara hiyo Rais Magufuli pia aliwataka viongozi wa Mkoa wa Kagera kufanyia kazi madai ya wananchi waliolalamikia kupata usumbufu katika kizuizi cha Kyaka jirani na Mto Kagera.

Hata hivyo aliwataka wananchi wa Mutukula kutambua kazi ya ulinzi na usalama inayofanywa na vyombo vya dola na aliwataka kutoa ushirikiano kwa viongozi na Serikali katika kuhakikisha mpaka huo unakuwa salama.

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa.
Aidha, Rais Magufuli aliwataka wananchi hao kuongeza juhudi katika shughuli za maendeleo zikiwemo kilimo na biashara. Alirejea agizo lake la kuutaka Mkoa wa Kagera kujenga soko la kimataifa katika maeneo ya jirani na mpaka huo ili wananchi wapate mahali pa kuuzia bidhaa zao kwa njia halali.
Wizara ya ujenzi yapewa mtihani mzito Wizara ya ujenzi yapewa mtihani mzito Reviewed by Zero Degree on 11/12/2017 03:46:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.