Loading...

Nyoni atangazwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Octoba


MCHEZAJI kiraka wa Simba, Erasto Nyoni ametangazwa kuwa mchezaji bora wa timu hiyo wa wa mwezi Oktoba.

Hiyo ni baada ya kuonyesha kiwango kikubwa kwenye mechi nne za Ligi Kuu Bara ambazo amezicheza Simba.

Nyoni alijiunga na Simba kwenye msimu huu wa ligi kuu akitokea Azam FC mara baada ya mkataba wake kumalizika.

Nyoni akicheza nafasi ya beki wa pembeni namba mbili hadi sasa tayari ameitengenezea klabu ya Simba mabao matano katika mechi za ligi ambazo amecheza.

Erasto ambaye anamudu kucheza nafasi nyingi uwanjani amekuwa chachu ya matokeo mazuri kwa timu ya Simba tangu asajiliwe akitokea Azam FC.

Mechi ambazo zimempa umaarufu katika mwezi uliopita hadi kupelekea kutwaa tuzo hiyo ya mchezaji bora wa mwezi ni dhidi ya Njombe Mji, Stand United, Mtibwa Sugar na Yanga, ambapo kati ya hizo walishinda mbili na kutoa sare mbili.
Nyoni atangazwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Octoba Nyoni atangazwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Octoba Reviewed by Zero Degree on 11/02/2017 05:19:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.