Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 2 Novemba, 2017
Nemanja Matic |
Thibaut Courtois anasema kwamba ilikuwa ni vigumu kwa Chelsea kumbakisha Nemanja Matic kikosini kwani alikuwa na hamu ya kuhamia Manchester United tangu mwanzo wa msimu wa majira ya joto. (Independent)
Madaktari wa klabu ya Chelsea watajaribu kupigania hali ya N'Golo Kante kwa haraka zaidi ili arejee mapema kikosini kucheza dhidi ya Manchester United Jumapili. (Telegraph)
Everton wako tayari kulipa pauni milioni 2.5 za kuachiliwa meneja wa Burnley Sean Dyche.
Meneja wa Tottenham, Mauricio Pochettinho |
Mauricio Pochettinho amekiri kwamba, hali ya jeraha la Toby Alderweireld ni mbaya baada ya beki huyo kuumia kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Real Madrid. (Sun)
Gareth Southgate hatamuita Jack Wilshere kwenye kikosi cha Uingereza kitakachocheza dhidi ya Ujerumani na Brazil na badala yake nafasi hiyo atapewa Harry Winks.
Nuno Espirito Santo anatathmini ikiwa atachukua nafasi iliyo Everton kufuata kufutwa kwa Ronald Koeman, lakini pia anatarajiwa kusalia Wolverhampton Wanderers. (Guardian)
Bodi ya Chelsea bado inaimani na Antonio Conte pamoja na kupoteza mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Roma.
Thibaut Courtois amesema kwamba, Chelsea hawatasalia katika vita ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza endapo watafungwa na Manchester United siku ya Jumapili.
Georginio Wijnaldum |
Hofu yatanda Liverpool baada ya Georginio Wijnaldum kupata majeraha na Phillipe Coutinho kuachwa nje kuelekea mechi yao na West Ham.
Arsene Wenger anasema anataka kumbakisha kimawazo Jack Wilshere hadi itakapofika mwezi Disemba ambapo anetegemea kuwa amekamilisha masula ya mkataba.
Jose Mourinho ana matamanio ya kumrejesha Andreas Pereira Manchester United. (Mirror)
Aliyekuwa meneja wa Rangers Ally McCoist, anapania kuongoza Sunderland kufuatia kufutwa kwa meneja Simona Grayson. (Daily Star)
Mshambuliaji wa Gremio, Luan, 24, ambaye alikuwa akitafutwa na Barcelona, Liverpool na Arsenal amesaini mkataba mpya na klabu hiyo ya Brazil hadi mwaka 2010. (Goal)
Mameneja Mauricio Pochettino wa Tottenham, Antonio Conte wa Chelsea na Jose Mourinho wa Manchester United huenda wakawa kwenye orodha ya wale wanaosakwa na Paris St-Germain. (Paris United)
Barcelona wana matumaini ya kumsajili mshambuliaji Timo Wener, 21, na mlinzi Dayot Upamecano, 19, kutoka RB Leipzig. (Mundo Deportivo)
Meneja wa Southend, Phil Brown anasema kuchukua usukani huko Sunderland inaweza kutumiza ndoto yake (Basildon)
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger, amekana uvumi wa kuihusisha Arsenal na kuhama kwa wing'a wa Monaco, Thomas Lemar. (Evening Standard)
Mauricio Pochettino anasema kwamba Tottenham ina uwezo wa kupambana na klabu yoyote baada ya kuifunga Real Madrid kwa mara ya kwanza. (Daily Mail)
Antonio Conte ana hofu kwamba Chelsea ina upungufu wa viongozi kwenye chumba cha kubadilishia nguo kufuatia usajili wa wachezaji uliopita. (Times)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 2 Novemba, 2017
Reviewed by Zero Degree
on
11/02/2017 04:51:00 PM
Rating: