Loading...

Rushwa yawafukuzisha kazi watumishi 71 wa Serikali


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imewafukuza kazi watumishi 71 na wengine 7 wakichunguzwa kwa tuhuma za rushwa huku watu wengine watatu ripoti zao zikiwa TAKUKURU na wawili wengine wao wameshafikishwa mahakamani tayari.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Mhandisi Patrick Mfugale akiwa mkoani Kigoma amethibitisha hilo na kusema kuwa watumishi hao ni wale waliokuwa wakihudumu katika mizani mbalimbali ya nchini na kudai kuwa wamekuwa wakikiuka taratibu mbalimbali.


"Wafanyakazi 71 tumewafukuza kazi lakini uchunguzi unaendelea kwa watu wengine saba ambao wao tunauhakika wanajiusisha na rushwa lakini kam tunavyojua uchuzi ni lazima pia wapo watu watatu ripoti zao tayari zipo TAKUKURU huku watu wengine wawili wao tayari wameshafikisha mahakamani" alisema Mfugale

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Mhandisi Patrick Mfugale amesema idadi ya wafanyakazi hao 71 waliofukuzwa ni toka mwezi Januari 2017 mpaka Oktoba mwaka huu.
Rushwa yawafukuzisha kazi watumishi 71 wa Serikali Rushwa yawafukuzisha kazi watumishi 71 wa Serikali Reviewed by Zero Degree on 11/02/2017 07:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.