Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 3 Novemba, 2017

Leon Goretzka
Leon Goretzka, mchezaji wa Shalke 04 ambaye anawindwa na klabu za Arsenal, Liverpool na Barcelona amepatwa na majeraha yatayomuweka nje kwa muda mrefu lakini klabu imesistiza kwamba lazima auzwe msimu huu. (Sun)

Kieran Tierney ameweka wazi nia yake ya kutaka kuendelea kusalia na klabu ya Celtic kwa kipindi chote kilichobakia katika maisha yake ya soka.

Kocha wa Burnley, Sean Dyche amesistiza kwamba, tetesi zililozeanea za yeye kuwaniwa na klabu ya Everton hazijawavunja moyo wachezaji wake. (Express)

Emre Can

Emre Can anakaribia kumalizana na Liverpool kufuatia mazungumzo yake na klabu juu ya mkataba mpya kutoonyesha uelekeo mzuri.

Charly Musonda
Charly Musonda ameiambia Chelsea kuwa anataka kuondoka mwezi Januari kwani maumivu ya kukaa benchi yamekuwa makubwa.

Luke Shaw anatazamia kurejea Southampton kwa kushtukiza ifikapo mwezi Januari kwa sababu ya kutofurahia kuwa Manchester United. (Mirror)

Kocha wa timu ya taifa ya Uingereza, Gareth Southgate ameonya kwamba haogopi kumuacha mchezaji yeyote nje ya kikosi baada ya kuwaacha nje wachezaji wengi wakongwe.


Klabu ya Wolfsburg imekiri kuwa na matumaini ya kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Divock Origi moja kwa moja. (Star)

Mauricio Pochettino achachamaa kufuatia tetesi zilizoenea kuhusu Real Madrid kumjumuisha Dele Alli kwenye orodha ya washambuliaji inaowahitaji ikiwa tayari wanamhitaji Harry Kane pia. 

Real Madrid itajaribu kumuajiri meneja wa Tottenham, Mauricio Pochettino kama chaguo lao la kwanza kuchukua mahali pake Zinedine Zidane. (Daily Mail)

Kiungo wa kati wa Manchester City Kevin de Bruyne, 26, anataka kucheza kwa muda mrefu katika klabu hiyo . (Sky Sports)


Harry Kane adai kwamba, Spurs wako vizuri kiasi cha kuweza kutwaa Ubingwa wa UEFA. (Telegraph)
Beki wa Marseille, Patrice Evra ameadhibiwa na UEFA kufuatia kutolewa uwanjani baada ya kuonekana akimpiga shabiki wa timu yake kichwani kabla ya mchezo wa Europa nchini Ureno.




Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho atamwachia beki wa klabu hiyo, Luke Shaw aondoke mwezi Januari.

Manchester City wanavizia kumsajili beki wa, Southampton, Ryan Bertrand kawenye dirisha la usajili mwezi, Januari.

Mmiliki wa Chelsea Roman Abrahamovic tayari ameamua kumfuta kazi meneja Antonio Conte. (Marca)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 3 Novemba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 3 Novemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 11/03/2017 01:40:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.