Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 10 Novemba, 2017

Nyota wa Timu ya Taifa ya Ubelgiji na Manchester City, Kevin de Bruyne
Eden Hazard amesma kuwa Kevin De Bruyne ndiye mchezaji bora kwenye Ligi Kuu ya Uingereza.

Manchester United ni miongoni mwa klabu ambazo ziko mstari wa mbele katika kuwania saini ya nyotwa wa Benfica, Umaro Embalo.

Klabu ya Manchester United wamemtaja beki wa Barcelona, Samuel Umtiti kuwa ni miongoni mwa wachezaji wanaowahitaji. (Daily Mail)

Sergio Ramos amesema kuwa baadhi ya wachezaji wa klabu ya Real Madrid hawapendezwi na tabia anazozionyesha Cristiano Ronaldo uwanjani.

Kiungo wa Ubelgiji, Dries Mertens anaweza kuhamia Ligi Kuu ya Uingereza siku zijazo lakini binafsi anasema anafurahia maisha akiwa Napoli. (Express)

Jack Butland
Goli kipa wa timu ya taifa ya Uingereza, Jack Butland atakuwa benchi kwa muda wa wiki sita baada ya kuvunja kidole chake akiwa kwenye mazoezi ya kujiandaa na mechi yao dhidi ya Ujerumani.

David Moyes anaweza kumuuza, Marko Arnautovic mwezi Januari baada ya kupewa kibali cha kuwaondoa wachezaji wote wa klabu ya West Ham wasio onyesha bidii.

Atletico Madrid wanategemewa kujaribu kumsajili kiungo wa Manchester United, Ander Herrera baada ya nyota huyo kugomea mkataba mpya Old Trafford.

West Ham wanaweza kujaribu kumsajili nyota wa klabu ya Bournemouth, Harry Arter.

Meneja wa Timu ya Taifa ya Ujerumani, Oliver Bierhoff
Oliver Bierhoff amesema kuwa, kiungo wa Schalke, Leon Goretzka atahamia Ligi Kuu ya Uingereza, ambapo Arsenal, Tottenham na Liverpool ni miongoni mwa klabu anazotazamia kujiunga nazo.

Frank Lampard amekataa kuzungumzia kuhusu uwezekano wa yeye kuchukua nafasi ya Michael Emenalo Chelsea. (Mirror)

Kwa mujibu wa ripoti zilizotolewa nchini Ufaransa, klabu ya Paris Saint-Germain ina mpango wa kumfanya Antonio Conte awe meneja wao mpya.


Roberto Mancini anahitaji apewe mshahara wa paundi milioni 15 kwa mwaka, safari kumi za ndege binafsi na nyingine 52 za kibiashara ili arejee Ligi Kuu ya Uingereza.

Nyota wa klabu ya Barcelona, Javier Mascherano amesema anataka kuondoka Nou Camp na kurejea katika klabu ya River Plate.

Wachezaji wa West Brom walishangazwa na kitendo cha meneja wao, Tony Pulis kuwapa ofa ya mapumziko ya wiki nzima baada ya kufungwa goli 1-0 na klabu ya Huddersfield.

Ashley Young alifikiri ni utani alipoambiwa amerejea kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza.

Kocha wa timu ya taifa ya Uingereza, Gareth Southgate amemtaja John Stones kuwa miongoni mwa mabeki bora Ulaya.

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger anasema ana furaha kubwa sana kusikia kwamba Lionel Messi atashiriki Kombe la Dunia 2018.

Steven Caulker ni miongoni mwa wachezaji wanaolipwa fedha nyingi wanaotarajiwa kuondoka QPR mwezi Januari. (Star)


Joleon Lescott
Joleon Lescott amemtaja mchezaji wa Manchester City, John Stones kuwa ndiye bora zaidi Uingereza.

Tony Adams ameitaka klabu ya Arsenal imuuze Alexis Sanchez mapema iwezekanavyo. (Sun)

Jose Mourinho anategemea kikosi cha Manchester United kitakuwa kimeimarika baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa kufuati Paul Pogba, Marcos Rojo na Michael Carrick kurejea mazoezini wiki hii.

Chris Coleman ameonyesha nia ya kutaka kuongeza mkataba wake na Wales baada ya kuzungumzia jinsi atakavyowapeleka wachezaji wake anaowakubali akiwemo na Gareth Bale - kwenye michuano ya 'China Cup' mwezi Machi mwakani. (Telegraph)
Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 10 Novemba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 10 Novemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 11/10/2017 05:09:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.