Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 14 Decemba, 2017

Golikipa wa klabu ya Athletic Bilibao, Kepa Arrizabalaga
Real Madrid wamekubali kulipa kiasi cha paundi milioni 22 kwa ajili ya kumnasa goli kipa wa Athletic Bilbao, Kepa Arrizabalaga - na hiyo inaweza kuwa ni ishara ya kwamba Thibaut Courtois na David de Gea kwa sasa hawako kwenye orodha yao ya wachezaji wanaotegemea kuwasajili mwezi Januari.

Andres Iniesta anasema kwamba hahofii matarajio ya klabu ya Real Madrid kumsajili aliyekuwa mchezaji mwezake Barcelona, Neymar, lakini anaweza kukereka endapo jambo hilo litafanikiwa.

Malaga wametoa ofa ya kumrejesha Sandro Ramirez, ambaye ameonyesha kiwango kidogo hadi hivi sasa tangu ajiunge na klabu ya Everton.

Meneja wa klabu ya Wolves, Nuno Espirito Santo ana uhakika kwamba nyota wake Leo Bonatini na Diogo Jota wanaoitumikia klabu yake kwa mkopo watakubali kusaini mkataba wa kudumu.

Dani Ceballos
Kwa mujibu wa ripoti za nchini Italia, klabu ya AC Milan imejiunga na Arsenal kwenye kinyang'anyiro cha kuwania saini ya chipukizi wa klabu ya Real Madrid, Dani Ceballos. (Mirror)

Mesut Ozil angependa kuhamia Manchester United badala ya Barcelona kama ataondoka Arsenal.

Kwa mujibu wa mmiliki wa klabu ya West Ham, David Sullivan, klabu hiyo itafanya usajili wa wachezaji wasiopungua wawili mwezi Januari.

Hofu ya kushuka daraja inachelewesha kukamilika kwa dili la Amanda Staveley kuinunua klabu ya Newcastle - hataki kumlipa mike Ashley pesa yote anayohitaji kama klabu itashuka daraja mwishoni mwa msimu wa 2017-18.

Mshambuliaji wa klabu ya Stevenage, Danny Newton, ambaye alisajiliwa kutoka V9 Academy, anafuatiliwa na QPR, MK Dons pamoja na Barnsley. (Daily Mail)

Klabu ya Bournemouth inahitaji kiasi cha paundi milioni 15 kumwachia straika wake, Benik Afobe.

Sime Vrsaljko
Liverpool wanatazamia kumsajili beki wa Atletico Madrid, Sime Vrsaljko mwenye thamani ya paundi milioni 22, lakini wanaweza kukumbana na ushindani kutoka klabu ya Napoli. (Sun)

Amanda Staveley ametoa ofa kwa mara ya pili kujaribu kuinunua klabu ya Newcastle United ingawa mmiliki wa klabu hiyo, Mike Ashley bado inaonekana hajawa tayari kuikubali na kumwomba aongeza ofa hiyo kwa mara nyingine tena. (Telegraph)

Juhudi za Shirikisho la Soka nchini Uingereza kubaini nani alikuwa chanzo cha mzozo baina ya wachezaji na viongozi wa Manchester United na Manchester City siku ya Jumapili zinaweza kugonga mwamba baada ya kugundulika kwamba hakuna kamera za CCTV kwenye ukanda ulio karibu na vyumba vya kubadilishia nguo Old Trafford. (Guardian)

Willian amewahakikishia mashabiki wa klabu ya Chelsea kwamba hataondoka mwezi Januari. (Evening Standard)

West Ham wameingia kwenye kinyang'anyiro cha kuwania  saini ya beki wa klabu ya Reading, Liam Moore.

Nia ya Rafa Benitez kuwanasa Danny Ings na Luke Shaw kutoka Liverpool inaweza kufanikiwa kutokana na kuchelewa kwa dili la kuuzwa kwa klabu ya Newcastle. (Express)

Kwa mujibu wa ripoti mbali mbali, Zinedine Zidane ana hamu sana Real Madrid ifanikishe usajili wa nyota wa klabu ya Chelsea, Eden Hazard.

Nyota wa Manchester United, Juan Mata anaamini thamani ya golikipa wa klabu hiyo, David de Ge haithaminiki nje ya Uingerezai. (Star)

Nahodha wa Barcelona Andres Iniesta anasema kwamba, mshambuliaji wa Liverpool, Philippe Coutinho atakuwa wa muhimu ikiwa watafanikiwa kumsajili mwezi Januari. (Goal)

Michy Batshuayi
Michy Batshuayi anaweza kuwa njiani kuondoka Chelsea kwa mkopo Januari na anaweza kuwa ndani ya ofa ambayo inategemewa kupelekwa Monaco kwa ajili ya kunasa Thomas Lemar. (Times)
Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 14 Decemba, 2017 Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 14 Decemba, 2017 Reviewed by Zero Degree on 12/14/2017 08:08:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.