Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 10 Decemba, 2017
Golikipa wa klabu ya Manchester United, David de Gea |
David de Gea hatalazimisha kuondoka Manchester United na badala yake ataicha klabu ya Real Madrid ikazanie jambo hilo.
Antonio Conte atamruhusu Michy Batshuayi kuondoka Chelsea kwa mkopo mwezi Januari.
Fulham wamefungua milango kwa Ryan Sessegnon kujiunga na Tottenham au Manchester United kwa kufanya juhudi ya kutafuta mbadala wake.
Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho watapata wasaa wa kumsajili Ivan Perisic mwezi Januari.
Ryan Giggs atafahamu kuhusiana na kama amefanikiwa kupata kazi ya kukinoa kikosi cha Wales mwezi Januari.
Meneja wa klabu ya Everton, Sam Allardyce anataka kumsajili Lamine Kone kutoka Sunderland na pia anatarajia kumpa mkataba mpya beki wake, Jonjoe Kenny.
Borussia Dortmund watamfukuza kazi Peter Bosz leo Jumapili, kwa mujibu wa ripoti zilizotoka.
Lewis Grabban anatarajiwa kurejea katika klabu yake ya Sunderland baada ya kuwa nje ya klabu hiyo kwa mkopo wa muda mrefu kabla hajauzwa kwa klabu ya Bournemouth.
Derby wanaingia katika vita ya kuwania saini ya kiungo wa Bolton, Josh Vela kwa paundi milioni 1.
Philippe Coutinho |
Philippe Coutinho ameiomba Liverpool impe uhakika wa kujiunga na klabu ya Barcelona.
Golikipa wa klabu ya Chelsea, Thibaut Courtois anategemea kuhamia nchini Uhispania huku akiendelea kukataa kusaini mkataba mpya na klabu yake.
Meneja wa Newcastle, Rafa Benitez ataitegemea klabu ya Liverpool mwezi Januari kuiimarisha safu yake ya ushambuliaji, akitazamia kuwasaji kati ya Danny Ings, Daniel Sturridge au Dominic Solanke kwa mkopo.
Real Madrid watajaribu kumsajili golikipa wa Tottenham, Hugo Lloris kama Spurs watashindwa kumshawishi asaini mkataba mpya.
Olivier Giroud anataka kuondoka Arsenal lakini ana matamanio makubwa ya kuibakiza familia yake katika Jiji la London hivyo anazipa matumaini klabu za West Ham na Crystal Palace.
Mike Ashley amepewa muda wa wiki mbili kukamilisha dili la kuiuza klabu ya Newcastle kwa Amanda Staveley.
Stoke City wana matamanio makubwa ya kumsajili wachezaji wa Timu ya Taifa ya Ghana, Daniel Opare na Edwin Gyasi - ambapo kwa sasa Opare anaichezea klabu ya Lens kwa mkopo wakati Gyasi yuko nchini Norway katika klabu ya Aalesund.
Jon Walters atakuwa huru kuondoka katika klabu ya Burnley kwa mkopo mwezi ujao baada ya kushindwa kulinda nafasi yake katika klabu hiyo. (Mirror)
Kiungo wa klabu ya Jack Wilshere ana amini kwamba anaweza kupigana hadi afanikiwe kurejea kwenye mipango ya klabu ya Arsenal. (Telegraph)
Jack Wilshere |
Arsenal wanatarajiwa kujaribu kumsajili chipukizi wa klabu ya Paris Saint-Germain, Goncalo Guedes.
Crystal Palace watamruhusu Pape Souare aondoke kwa mkopo mwezi January, huku klabu za Marseille na Galatasaray zikiwa na matamanio makubwa ya kumsajili raia huyo wa Senegal.
Sergio Romero anataka kuondoka Manchester United mwezi January kulinda nafasi yake katika kikosi cha Argentina kwenye Kombe la Dunia. (Daily Mail)
Golikipa wa klabu ya Chelsea, Thibaut Courtois anategemea kuhamia nchini Uhispania huku akiendelea kukataa kusaini mkataba mpya na klabu yake.
Jose Mourinho anajiandaa kuweka rekodi ya klabu kwa kuandaa ofa ya paundi milioni 95 kumnasa kiungo wa Lazio, Sergej Milinkovic-Savic. (Express)
Jack Wilshere amekiri kutoelewa nini kitatokea juu ya 'future' yake katika klabu ya Arsenal akiwa amebakiwa na miezi sita pekee kwenye mkataba wake wa sasa na klabu hiyo. (Observer)
Jack Wilshere amekiri kutoelewa nini kitatokea juu ya 'future' yake katika klabu ya Arsenal akiwa amebakiwa na miezi sita pekee kwenye mkataba wake wa sasa na klabu hiyo. (Observer)
Rafa Benitez |
Watford wanatarajiwa kumsajili chipukizi wa klabu ya IFK Gothenburg, Pontus Dahlberg kama mbadala wa golikipa wao, Heurelho Gomes. (Star)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumapili Tarehe 10 Decemba, 2017
Reviewed by Zero Degree
on
12/10/2017 03:46:00 PM
Rating: