Loading...

Ukarabati umeanza kwa mabweni ya UDSM yalioonesha nyufa


Wakala wa Majengo nchini (TBA) umefanya ukarabati wa majengo ya mabweni ya chuo kikuu cha Dar es salaam ambayo hivi karibuni yalionekana kuweka nyufa.

Picha zinazoonyesha nyufa hizo zikiwa zimezibwa
Vyombo vya habari vilivyofika kwenye eneo hilo vilikuta tayari mafundi wameshaweka plasta ili kuziba nyufa hizo, ambazo Mkurugenzi Mkuu wa TBA Elius Mwakalinga alisema zimesababishwa na 'expansion joint' ambayo ni kitu cha kawaida kwenye ujenzi.

Hivi karibuni kulisambaa picha za majengo zikionyesha kuwa na nyufa, huku yakiwa hayajamaliza mwaka tangu yakabidhiwe na kuanza kutumika na wanafunzi, kitendo kilichosababisha mpiga picha hizo ashikiliwe na polisi.
Ukarabati umeanza kwa mabweni ya UDSM yalioonesha nyufa Ukarabati umeanza kwa mabweni ya UDSM yalioonesha nyufa Reviewed by Zero Degree on 12/13/2017 06:31:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.