Waziri wa Fedha aeleza hali ya ukuaji wa uchumi
Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango alipokuwa akizungumza kuhusu hali ya uchumi wa Taifa, utekelezaji wa bajeti mwaka 2017/2018.
“Katika nusu ya kwanza ya mwaka huu pato la taifa limekuwa kwa asilimia 6.8 ukilinganisha na asilimia 7.7 katika kipindi kama hicho mwaka 2016, sasa hapa nataka nifafanue kidogo kwa wale ambao sio wataalamu ukuaji wa uchumi hauendi wima au kama mstari ulionyooka hata kidogo,” alisema Dk. Mpango.
“Mara nyingi wachumi wanapochora ukuaji wa pato la taifa unaenda kama mawimbi hivi tena mawimbi yenye hayalingani na sababu yake ni rahisi kwasababu kwa mfano kilimo kina msimu amabo ndio tunavuna lakini pia nikitoa mfano mwingine kama utalii kuna msimu wa watalii wengi na kuna wakati ni low season . Haiwezekani uchumi ukawa unapanda .”
Waziri wa Fedha aeleza hali ya ukuaji wa uchumi
Reviewed by Zero Degree
on
12/30/2017 12:01:00 PM
Rating: