Loading...

TCRA yatangaza kushusha gharama za mawasiliano ya simu

Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba
Mamlaka ya Mawasiliano nchini Tanzania (TCRA), imetangaza kupunguza kiwango cha gharama za mawasiliano ya simu nchini Tanzania kutoka 26.96 kwa dakika moja mwaka huu hadi 15.60 kuanzia 2018.

Akitangaza punguzo hilo la viwango vipya vya mawasiliano ya simu ambavyo vitaanza kutumika Januari Mosi, 2018, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba amesema viwango hivyo vitaendelea kupungua kila mwaka hadi kufikia shilingi 2 mwaka 2022

Aidha Mhandisi Kilaba amesema hatua hiyo itasaidia kuongeza idadi ya watumiaji wa matumizi ya simu na kuongeza pato la watoaji huduma wa mitandao ya simu na taifa kwa ujumla.
TCRA yatangaza kushusha gharama za mawasiliano ya simu TCRA yatangaza kushusha gharama za mawasiliano ya simu Reviewed by Zero Degree on 12/30/2017 11:51:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.