Loading...

Baada ya Sanchez, hawa hapa wachezaji wengine 2 walioko kwenye rada za Mourinho


Manchester United imegeukia kwa Carlos Soler na Julian Weigl baada ya kuwa dili la uhamisho wa Alexis Sanchez limekamilika mwezi huu.

Alexis Sanchez alitangazwa rasmi kuwa mchezaji wa Manchester United siku ya Jumatatu akitokea Arsenal, huku Henrikh Mkhitaryan akielekea 'The Gunners'.

Carlos Soler, 21
Inasemekana kwa sasa vigogo hao wa Ligi Kuu ya Uingereza wanatazamia kuongeza nguvu katika safu yao ya kiungo, huku chaguo la kwanza la Jose Mourinho ikiaminika kuwa ni kiungo wa klabu ya Valencia, Carlos Soler na 
Julian Weigl wa Borussia Dortmund.

Julian Weigl, 22
Ripoti zinadai kwamba, klabu hiyo ya Uingereza ina uhakika wa kukamilisha usajili wa wawili hao mwezi huu.
Baada ya Sanchez, hawa hapa wachezaji wengine 2 walioko kwenye rada za Mourinho Baada ya Sanchez, hawa hapa wachezaji wengine 2 walioko kwenye rada za Mourinho Reviewed by Zero Degree on 1/24/2018 11:44:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.