Mrema atinga polisi kuripoti tukio la kuzushiwa kifo
Mwenyekiti wa Bodi ya Parole, Augustine Mrema akitoka kituo cha polisi |
Mrema amedai waliozusha taarifa hizo walitaka wananchi wasisikilize mazungumzo aliyofanya Rais Magufuli na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa badala yake wajadili kifo chake.
Pamoja na hayo Mrema amesema kwamba malalamiko yake mengine ni kwamba alipata usumbufu uliomfanya ashindwe kwenda mkoani Kilimanjaro ambapo alipanga kwenda kwa ajili ya kuwafanyia ibada wazazi wake waliokwisha tangulia mbele za haki ikiwa ni pamoja na kufanya misa ya shukrani kwa kupona ugonjwa uliokuwa ukimsumbua tangu kipindi cha uchaguzi.
Mrema amesema kwamba waliosambaza taarifa hizo walisababisha mtafaruku kwa famiia na watu wengine ambao walianza kupata masikitiko kutokana na taarifa hizo ambazo zilianza kusambazwa siku ya Jumanne, Januari 9
"Lengo lao lilikuwa kuvuruga mkutano wa Lowassa na Rais ambao ulifanyika Ikulu, hivyo walikuwa hawataki watu wafuatilie ndiyo walijua wakisema Mrema amekufa watu wangekuwa bize na mimi kwa sababu mimi ni mashuhuri, na wasingehangaika na kile ambacho rais aliongea na Lowassa" Amesema Mrema.
Pamoja na hayo Mrema amesema kwamba malalamiko yake mengine ni kwamba alipata usumbufu uliomfanya ashindwe kwenda mkoani Kilimanjaro ambapo alipanga kwenda kwa ajili ya kuwafanyia ibada wazazi wake waliokwisha tangulia mbele za haki ikiwa ni pamoja na kufanya misa ya shukrani kwa kupona ugonjwa uliokuwa ukimsumbua tangu kipindi cha uchaguzi.
Mrema amesema kwamba waliosambaza taarifa hizo walisababisha mtafaruku kwa famiia na watu wengine ambao walianza kupata masikitiko kutokana na taarifa hizo ambazo zilianza kusambazwa siku ya Jumanne, Januari 9
Mrema atinga polisi kuripoti tukio la kuzushiwa kifo
Reviewed by Zero Degree
on
1/12/2018 06:23:00 PM
Rating: