Loading...

Serikali yataka zao la Mbaazi lianze kuliwa kwenye Magereza na shule za sekondari

Waziri wa kilimo, Mhe. Charles Tizeba
Serikali imeagiza zao la Mbaazi lianze kuliwa katika Magereza na shule za sekondri badala ya kutegemea Maharagwe pekee lengo likiwa kuongeza thamani ya zao hilo ambalo limeyumba na kukosa soko kutokana na kutegemea masoko ya nje pekee.

Waziri wa kilimo Mhe. Charles Tizeba ametoa agizo hilo mkoani Mtwara wakati akipokea taarifa ya mkoa ambapo amesema hilo ni fundisho na serikali haiwezi kutegemea masoko ya nje pekee.

Amesema maeneo kama Magereza na shule za sekondari hazina budi kutumia kitoweo hicho badala ya kutegemea maharagwe pekee lengo likiwa kuongeza thamani ya zao hilo ambalo kwa sasa halina soko.

Hata hivyo amesema serikali kwa sasa inafanya mikakati ya kupata masoko katika nchi zingine ikiwemo Morishas baada ya nchi ya India ambayo ilikuwa mnunuzi mkuu wa zao hilo kuzalisha kwa wingi zao hilo katika msimu uliyopita.

Akiwa mkoani Mtwara Mhe. Tizeba ametembelea pia kituo cha utafiti wa kilimo Naliendele ili kujionea shughuli zinazofanywa na kituo hicho, sambamba na kutembelea bandari ya Mtwara kujionea usafirishaji wa Korosho kwenda nje ya nchi unavyo fanyika.
Serikali yataka zao la Mbaazi lianze kuliwa kwenye Magereza na shule za sekondari Serikali yataka zao la Mbaazi lianze kuliwa kwenye Magereza na shule za sekondari Reviewed by Zero Degree on 1/16/2018 07:50:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.