Loading...

Uhuru Kenyatta atangaza Sehemu ya Baraza lake jipya la Mawaziri Kenya

Rais Uhuru Kenyatta alitangazwa kuwa mshindi wa kiti cha urais baada ya uchaguzi wa marudio nchini Kenya akiwa na kura 7,483,895 sawa na 98%.
Miezi miwili baada ya kuhifadhi kiti chaka cha Urais, Uhuru Kenyatta ameanza kuunda baraza lake jipya kwa kuwateua tena mawaziri sita wa zamani.

Akitangaza sehemu ya baraza lake jipya, Rais huyo wa Kenya pia amependekeza wanasiasa wawiwili kuchukua nafasi za uwaziri.

Kinachoshangaza wadadisi wa maswala ya kisiasa ni kutangazwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka wa Kenya, Bw KeriakoTobiko kuwa waziri. Hii ni mara tu baada ya Uhuru Kenyatta kutangaza kwamba amekubali maombi ya Bwana Tobiko ya kujiuzulu kama Mkurugenzi wa Mashtaka wa Kenya.

Waliohifadhiwa katika baraza hilo jipya ni Waziri wa Usalama wa ndani Fred Matiangi, Waziri wa fedha Bwana Henry Rotich, Waziri wa Utalii Najib Balala, na Bwana Joseph Mucheru akihifadhi wadhifa wake wa Waziri wa Teknolojia na Habari. Waziri wa Mawasiliano amesalia kuwa Bwana James Macharia na Waziri wa Kawi ni Bwana Charles Keter.

Wanasiasa walipoendekezwa na rais kushikilia wadhifa wa uwaziri ni aliyekuwa Seneta wa Jimbo la Turkana, John Munyes na aliyekuwa Gavana wa Marsabit, huko Mashariki mwa Kenya, Ukur Yatani.

Kiongozi huyo wa Kenya anayehudumu kwa kipindi chake cha pili na cha mwisho kama rais amesema bado yuko katika harakati ya kubuni baraza lake kamili .

Katiba ya Kenya inasema kwamba baraza la mawziri sharti liwe na mawaziri kati ya 14 na wasizidi 22.

Rais Uhuru Kenyatta aliingia madarakani kwa awamu ya pili baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa kiti cha urais baada ya uchaguzi wa marudio nchini Kenya mwezi Oktoba mwaka 2017.
Uhuru Kenyatta atangaza Sehemu ya Baraza lake jipya la Mawaziri Kenya Uhuru Kenyatta atangaza Sehemu ya Baraza lake jipya la Mawaziri Kenya Reviewed by Zero Degree on 1/06/2018 09:30:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.