Loading...

Usain Bolt amesaini mkataba kucheza Soka


Bingwa wa zamani wa dunia wa mbio za mita 100 Mjamaica Usain Bolt, leo amesaini mkataba wa kushiriki kwenye mechi ya soka inayoandaliwa na UNICEF SOCCER AID mwezi Juni.

Bolt ameshangaza watu wengi baada ya kutangaza kuwa leo atasaini mkataba na klabu ya soka huku wengi wakiamini huenda angejiunga na timu ya Mamelodi Sondowns ya Afrika Kusini ambayo hivi karibuni alionekana akifanya nayo mazoezi.

Bolt, mwenye umri wa miaka 31, amekuwa akiweka wazi juu ya mapenzi yake na mchezo wa soka hivyo watu wengi waliamini leo atatangaza kujiunga na timu ya soka.

Mkata upepo huyo amewahi kuzitaja timu za Real Madrid na Manchester United na Real Madrid kuwa anatamani kuzichezea huku mwezi Januari pia akitangaza kuwa mwezi Machi ataanza kufanya mazoezi na kikosi cha Borussia Dortmund.

Katika mechi hiyo ambayo itachezwa kwenye uwanja wa klabu ya Manchester United, Old Trafford Juni 10, anatarajiwa kushiriki pia mwanamuziki nyota Robbie Williams.
Usain Bolt amesaini mkataba kucheza Soka Usain Bolt amesaini mkataba kucheza Soka Reviewed by Zero Degree on 2/27/2018 09:50:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.