Loading...

Ajali yaua watu 7 mkoani Kigoma


Watu 7 wamefariki katika ajali iliyohusisha gari aina ya Scania Lori iliyotokea katika kijiji cha Mkongoro mkoani Kigoma.

Chanzo cha ajali hiyo kimeelezwa kuwa dereva wa lori hilo alishindwa kulimudu gari wakati akishuka kwenye mteremko uliokuwa na kona kali, na kumgonga mtembea kwa miguu na kisha kupinduka na kusababisha vifo vya watu hao saba.

Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma, Martin Otieno amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva kushindwa kuimudu gari kwenye mteremko.


Amesema ajali hiyo imetokea saa tatu asubuhi katika Mlima wa Kasagamba ambapo lori lenye namba T741AAB lilianguka na kusababisha vifo vya watu saba akiwamo dereva wa gari hiyo aliyefahamika kwa jina la Siri Hamis (43) mkazi wa Singida pamoja na utingo wake aliyefahamika kama Ramadhani Saidi (23).

“Katika gari hiyo walikuwa wamebeba mizigo na watu wanne mmoja mwanamke na watatu wanamume ambapo wengine waliofariki na majina yao hayakufahamika mara moja.

“Ajali hiyo pia imesababisha kifo cha mwanafunzi aliyefahamika kwa jina la Eliakimu Samsoni (15 ), aliyekuwa akitembea kwa miguu kuelekea shuleni na gari hilo kumgonga akiwa anatembea,” amesema Kamanda Otieno.
Ajali yaua watu 7 mkoani Kigoma Ajali yaua watu 7 mkoani Kigoma Reviewed by Zero Degree on 3/21/2018 12:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.