Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 21 Machi, 2018

Paulo Dybala
Diego Simeone alioneka akipata chakula cha jioni pamoja na mshambuliaji wa Juventus, Paulo Dybala, huku mshambuliaji wa klabu ya Atletico Madrid, Antoine Griezmann akijiandaa kukamilisha uhamisho wake kwenda Barcelona.

Aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid, Raul Gonzalez ameamua kujaribu bahati yake kwenye ukufunzi. (Marca)
 
Mshambuliaji wa klabu ya Bordeaux, Malcom, ambaye anawindwa na Arsenal pamoja na Tottenham amesema kuwa anataka kuichezea klabu moja wapo yenye jina kubwa barani Ulaya. (Sky Sports)

Kushindwa kuzungumza lugha ya kijerumani vizuri inaweza kuwa sababu kwa Bayern Munich kuamua kuachana na meneja wa klabu ya Tottenham, Maurcio Pochettino.

Bayern Munich wanatamani kumsajili chipukizi wa klabu ya Hamburg, Jann- Fiete Arp. (Bild)

Jose Mourinho anataka kuuza karibu wachezaji nane wa Manchester United kwenye majira ya joto ili akusanye fedha kwa ajili ya uhamisho wa Marco Verratti, Toni Kroos, Toby Alderweireld na Samuel Umtiti.

Beki wa klabu ya West Ham, Declan Rice anasema kuwa anachoka ni kuichezea timu ya taifa ya Jamuhuri ya Ireland na hatakuwa tayari kuitikia wito wowote wa mazungumzo na meneja wa Uingereza, Gareth Southgate.

Manchester United wana mpango wa kutoa karatasi za nyimbo kwa mashabiki katika mechi za nyumbani ili kuboresha hali ya kimchezo iliyopo katika dimba la Old Trafford. (Times)

Beki wa klabu ya Manchester United, Marcos Rojo anasema kuwa Jose Mourinho alimwambia asimchezee vibaya Alexis Sanchez wakati wa mazoezi kwa sababu ya tofauti zao za muda mrefu.

Manchester United wameachana na mpango wao wa kutaka kumsajili straika wa Atletico Madrid, Antoine Greizmann na badala yake watarejesha mashambulizi yao kwa nyota wa Real Madrid, Gareth Bale kwenye majira ya joto.

Angel Di Maria
Manchester United wanahofu kwamba Alexis Sanchez anapata wakati mgumu sana kuendana klabu yao na kuhofia kujirudia kwa hali iliyomkuta Angel Di Maria. (Daily Mail)

Timu ya taifa ya Wales imefanikiwa kukwepa faini ya pauni 100,000 ambayo ingelazimika kulipa kama Gareth Bale asingeenda kushiriki michuano ya China Cup.

Anthony Martial anaonekana ni miongoni mwa watakaoongezeka kwenye orodha ya wachezaji watakao ondoka kwenye majira ya joto. (Express)

Arsenal wanfanya mpango wa kutoa ofa ya pauni milioni 45 kwa ajili ya kiungo wa Ufaransa, Nabil Fekir baada ya wakala wake kudai nyota huyo anaweza kuondoka Lyon kwenye majira ya joto.

Jack Wilshere ataipa nafasi nyingine Arsenal ya kumpa ofa ya mkataba mpya, akiwa tayari ameshakataa kusaini mkataba mwingine ambao uliambatana na kupunguzwa kwa mshahara wake wa pauni 120,000 kwa wiki. (Sun)

klabu ya Bayern Munich itajaribu kumshawishi meneja wa Tottenham, Mauricio Pochettino atue Bundesliga baada ya kuzikonga nyoyo za vigogo wa klabu hiyo ya Ujerumani kwenye Ligi ya Mabingwa.

Kiungo wa Liverpool, Emre Can anasema kuwa hajutii kuondoka Bayern Munich wakati Pep Guardiola alipokuwa mkufunzi wa vigogo hao wa Bundesliga.

Shirikisho la Soka la Uingereza (FA) linatarajiwa kumchunguza mshambuliaji wa Man United, Zlatan Ibrahimovic juu ya kuhusika na kampuni mpya ya michezo ya kubashiri kuona kama amekiuka kanuni na taratibu zao.

Tottenham imekuwa ikimfuatilia kwa karibu zaidi beki wa Bayer Leverkusen, Jonathan Tah anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 25 kuelekea usajili wa kwenye majira ya joto.

Chelsea imeingia kwenye kinyang'anyiro cha kuwania saini ya beki wa klabu ya Tottenham, Toby Alderweireld. (Mirror)

Toby Alderweireld
Tottenham imekataa tamaa kwa Toby Alderweireld lakini itahitaji walau kiasi cha pauni milioni 42 ili kumwachia beki huyo kwenye majira ya joto.

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amemfanya kiungo wa klabu ya Schalke 04 Max Meyer, kuwa chaguo lake la kwanza kwenye majira ya joto.

Joao Mario anataka kuufanya uhamisho wake wa mkopo kutoka Inter kwenda West Ham uwe wa kudumu kwenye majira ya joto, huku wagonga nyundo hao wakiwa na kipengele cha kumsajili moja kwa moja kiungo huyo kutoka Ureno kwa pauni milioni 27 kwenye mkataba wao. (Star)

Beki wa klabu ya Chelsea, Andreas Christensen anasema kuwa John Terry ana mchango mkubwa sana katika mafanikio yake Stamford Bridge.

Straika wa Atletico Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa Antoine Griezmann amesema kuwa ataamua juu ya hatima yake katika klabu yake kabla ya Kombe la Dunia. (ESPN

Beki wa Tottenham, Eric Dier atatumika kama beki wa kati wa timu ya taifa ya Uingereza kwenye mechi zao za kirafiki dhidi ya Uholanzi na Italia.

Paul Pogba anapanga kutoa maelezo ya kina kwa Didier Deschamps juu ya matatizo anayopitia katika klabu ya Manchester United wakati atakapofanya mazungumzo na kocha huyo wa timu ya taifa ya Ufaransa wiki hii.

Chris Gunter amekanusha taarifa zinazodai kuwa wachezaji wa timu ya taifa ya Wales walimwomba Chris Coleman asiondoke. (Telegraph)

Luke Shaw
Ashley Young ana amini Luke Shaw atakuja kuwa miongoni mwa mchezaji wazuri duniani lakini amemuonya mchezaji mwenzake wa Manchester United kwamba hilo litawezekana kwa kufanya kazi kwa bidii. (Guardian)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 21 Machi, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 21 Machi, 2018 Reviewed by Zero Degree on 3/21/2018 11:27:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.