Loading...

Chelsea na Real Madrid zinaongoza mbio za kuwania saini ya straika huyu kutoka Bundesliga

Chelsea na Real Madrid ndio vinara katika mbio za kuwania saini ya mshambulaji matata kutoka klabu ya Bayern Munich na Timu ya Taifa ya Poland, Robert Lewandowski
Chelsea na Real Madrid ziko mstari wa mbele katika mbio za kuwania saini ya Robert Lewandowski kwenye majira ya joto na kwa mujibu wa ripoti mbalimbali, mshambuliaji huyo wa Bayern Munich yuko tayari kundoka Ujerumani.

Raia huyo wa Poland ana rekodi ya kushangaza akiwa na vigogo hao wa Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga). Amefunga magoli 139 katika mechi 181 akiwa na klabu hiyo.

Amekuwa akihusishwa na kuondoka Bayern Munich kwa muda wa miezi kadhaa, hata hivyo, kumekuwa na klabu kadhaa zenye majina makubwa kutoka Ulaya ambazo zinahitaji saini yake.

Ripoti zinada Lewandowski yuko tayari kuondoka kwenye majira ya joto kama nafasi nzuri itajitokeza. Inadaiwa Chelsea na Real Madrid ndio zinaongoza kwa kuwa na nafasi kubwa ya kufanikisha uhamisho wa stariaka huyo.

Mshambuliaji huyo mwenye uzoefu mkubwa anaweza kuichukua hii kama nafasi yake ya mwisho kuweza kukamilisha uhamisho mwingine mkubwa katika historia yake ya soka na inasemekana chaguo lake la kwanza ni Real Madrid.

Mshambuliaji wa klabu ya Bayern Munich na Timu ya Taifa ya Poland, Robert Lewandowski
Lewandowski anakadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 80, lakini klabu ya Bayern Munich haina mpango wa kumuuza mshambuliaji huyo licha ya kwamba vilabu vingi vinamhitaji.

Manchester United imeripotiwa kuwa na nia ya kumsajili Lewandowski. Lakini, Jose Mourinho ataangazia zaidi usajili wa viungo kwenye majira ya joto.
Chelsea na Real Madrid zinaongoza mbio za kuwania saini ya straika huyu kutoka Bundesliga Chelsea na Real Madrid zinaongoza mbio za kuwania saini ya straika huyu kutoka Bundesliga Reviewed by Zero Degree on 3/09/2018 05:13:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.