Loading...

Mahakama yaamuru Shilole alipe Sh milioni 14/= kwa kusababisha hasara


MAHAKAMA ya Mwanzo ya Kinondoni jijini Dar es Salaam imemhukumu msanii wa bongo fleva na filamu, Zuwena Mohamed 'Shilole’ alipe faini ya Sh milioni 14/- kwa kusababisha hasara.

Akisoma hukumu hiyo, hakimu wa mahakama ya Mwanzo Kinondoni, A. P. Mshingwa amesem,a Shilole amekuwa akitumiwa mwito mara kwa mara na mahakama afike kusikiliza kesi hiyo lakini alikuwa akikaidi kufanya hivyo hadi mahakama ilipomuandikia mwito mwingine kwenye gazeti moja nchini lakini hakufika.

Imedaiwa mahakamani hapo kwamba, Shilole ilikuwa akatumbuize kwenye onesho lililoandaliwa na Mary Mussa Mbagala mwaka jana, lakini hakufika jambo lililosababisha hasara kwa mwandaaji.

Shilole anadaiwa kulipwa Sh milioni tatu kwa ajili ya kutumbuiza kwenye mkesha wa Pasaka mwaka jana katika ukumbi wa Heineken uliopo Mbagala Kijichi Dar es Salaam, lakini hakufika, hali iliyosababisha mashabiki kufanya vurugu na kuharibu mali mbalimbali.

Baada ya hukumu hiyo, Mahakama imemuamuru Shilole azilipe fedha hizo haraka ndani ya wiki moja vinginevyo mali zake zitaanza kukamatwa.
Mahakama yaamuru Shilole alipe Sh milioni 14/= kwa kusababisha hasara Mahakama yaamuru Shilole alipe Sh milioni 14/= kwa kusababisha hasara Reviewed by Zero Degree on 3/01/2018 07:36:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.