Loading...

Msumbiji: Akamatwa kwa kujaribu kumfufua mfu


Kasisi mmoja nchini Msumbiji amejipata mikononi mwa polisi baada ya kujaribu kumfufua mwanamume mmoja eneo la kati la Msumbiji bila mafanikio.

Kasisi huyo alidai kuwa roho mtakatifu alimwambia alisafiri hadi katika hospitali ya Chimoio katika jimbo la Manica, kufanya muujiza huo.

Kasisi huyo ambaye aliyedai kuwa na uwezo wa kufanya muujiza huo aliweza kuikonga mioyo ya maafisa wa hospitali hadi wakamruhusu aingie ndani ya chumba cha maiti kuutekeleza muujiza wake.

Hata hivyo baada ya siku mbili za maombi makali, hakuweza kabisa kurejesha uhai wa marehemu.

Haikuishangaza familia ya marehemu.

Dada yake marehemu - ambaye hakutaka jina lake litajwe - aliwaambia waandishi wa habari:

"Kasisi aliomba, akaomba na kuomba hadi akanena kwa lugha. Alizungusha kichwa cha marehemu huku na kule huku akiomba.

"Lakini hakuna hata sehemu ya marehemu kaka yangu iliyoweza kutikisika. Wakati mmoja kasisi alipaza sauti akisema: 'amka, kijana wa Mungu!"

"Hatukuamini kasisi angefanya muujiza wowote. Hii ni kwa sababu hakuwahi, hata wakati mmoja, kuthibitisha uwezo wake wa kumrejeshea mfu uhai wake.

"Tangu wakati huo kasisi alikamatwa na yuko mikononi mwa polisi akishtakiwa kwa kosa la kumkosea heshima mfu."
Msumbiji: Akamatwa kwa kujaribu kumfufua mfu Msumbiji: Akamatwa kwa kujaribu kumfufua mfu Reviewed by Zero Degree on 3/28/2018 12:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.