Loading...

Roma wanataka wachezaji watatu wa Real Madrid kwenye majira ya joto


Roma wako nafasi ya nne kwenye ligi kwa sasa na wanataka kuongeza nguvu mpya kwenye majira ya joto ili kushindania taji la Serie A msimu ujao. Tayari wameanza mchakato wa kusaka wachezaji wazuri na wanapanga kusajili nyota kadhaa kutoka klabu ya Real Madrid.
Kwa mujibu wa taarifa ya Diario Gol, Roma wako tayari kulipa karibu pauni milioni 90 kusajili wachezaji watatu wa Real Madrid. Mkurugenzi wa michezo wa vigogo hao wa Italia, Rodríguez Verdejo 'Monchi' anakusudia kuwasajili wachezaji watatu akiwemo Lucas Vazquez, Mateo Kovacic na Nacho Fernandez. Anataka kutumia hamu ya wachezaji hao kupata muda wa kutosha uwanjani kwa manufaa yake na kati yao wote watatu hakuna hata mmoja aliyefanikiwa kuipata nafasi hiyo akiwa Santiago Bernabeu.

Mateo Kovacic
Kovacic amekuwa akihusishwa na kuondoka Madrid kwenye majira ya joto. Yeye mwenyewe tayari ameshazungumzia hamu yake ya kuondoka kwa sababu ya kupigwa benchi na anaweza kwenda Italia.

Nacho Fernandez
Sawa na Nacho. Amekuwa akijitahidi kuonyesha uwezo mkubwa kila anapopewa nafasi lakini bado hana uhakika kwenye kikosi cha kwanza mbele ya Sergio Ramos na Raphael Varane. Nyota huyo pia amekuwa akihusishwa na kuondoka kwenye majira ya joto.

Lucas Vazquez
Lucas pekee, ndiye hajahusishwa na uhamisho wowote. Lakini bado anaweza kushawishika kuondoka kwani anatambua kwamba Cristiano Ronaldo na Gareth Bale ni wachezaji wakubwa na hana uwezo wa kushindania namba na wawili hao bali ataishia kucheza mechi zisizokuwa na umuhimu.
Monchi anaamini kwamba, kiasi alichotoa kama ofa kinatosha kuishawishi Real Madrid kuwauza wachezaji hao kwenye majira ya joto. Vigogo hao wa La Liga pia wanapanga kununua wachezaji wapya kwenye majira ya joto na wanaweza kutumia fedha hizo kuimarisha kikosi cha zaidi.
Roma wanataka wachezaji watatu wa Real Madrid kwenye majira ya joto Roma wanataka wachezaji watatu wa Real Madrid kwenye majira ya joto Reviewed by Zero Degree on 4/12/2018 08:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.