Loading...

Ajali ya gari yaua maofisa watatu wa TIC


MAOFISA watatu wa Kituo cha Uwekezaji cha nchini (Tanzania Investment Center (TIC) wamefariki dunia katika ajali ya gari usiku wa kuamkia leo maeneo ya Chalinze wakiwa njiani kuelekea jijini Dodoma.

Waliofariki ni Saidi Amiri Moshi (Kaimu Mkurugenzi wa Research zamani Corporate Affairs), Zacharia Kingu (Kaimu Mkurugenzi wa Corporate Affairs zamani Investment Promotion) na Martin Masalu (Meneja Research).

Waliopata majeraha ni wawili yaani Godfrey Kilolo (Meneja wa Sheria) na dereva wa gari hilo aliyejulikana kwa jina moja tu la Priscus. Wote walikuwa wakielekea Dodoma kwa ajili ya mkutano ambao unatakiwa kufanyika leo Jumanne jijini humo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani amethibitisha kutokea kwa ajali maeneo ya Msoga wilayani Chalinze na kusababisha vifo vya watu wawili na mmoja kujeruhiwa.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Jonathan Shana amesema ajali hiyo imehusisha gari ya serikali STK 5923 aina ya Toyota land cruiser lililongana na Scania T620 AQV ambaye dereva wake alitoweka kusikojulikana na waliofariki ni watendaji wa kituo cha uwekezaji TIC waliokuwa wakielekea Jijini Dodoma.

Kamanda Shana amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa Gari ndogo alikuwa akikwepa mashimo yaliyokuwa barabarani na kwakuwa lilikuwa kwenye mwendo mkali liliparamia lori.
Ajali ya gari yaua maofisa watatu wa TIC Ajali ya gari yaua maofisa watatu wa TIC Reviewed by Zero Degree on 5/22/2018 08:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.