Loading...

Rais Nkurunziza kuiongoza Burundi hadi mwaka 2034

Rais Pierre Nkurunziza
Wapiga kura nchini Burundi wameunga mkono mabadiliko ya katiba ambayo yatamruhusu Rais wa nchi hiyo kusalia madarakani hadi mwaka 2034.

Kwa mujibu wa matokeo ya kura za mabadiliko ya katiba yaliyotangazwa na Tume ya uchaguzi ya nchi hiyo siku ya jana yameonesha kuwa asilimia 73 ya wapiga kura wote wameunga mkono mabadiliko hayo ya katiba.

Mabadiliko hayo ya katiba ni pamoja na kurefusha muhula wa Rais kutoka miaka mitano hadi saba na kwa mabadiliko hayo yatamfanya Rais Nkurunziza kugombea tena kipindi cha mihula mingine miwili baada ya awamu yake sasa kumalizika mwaka 2020.

Hata hivyo, Serikali ya Marekani kupitia kwa Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Heather Nauert imesema kuwa mchakato wa kura za maoni juu ya mabadiliko hayo ulikuwa na dosari nyingi na haukuwa wa uwazi.

“Mchakato wa kura za maoni ulikuwa na dosari ya kutokuwepo uwazi, kufungiwa kwa vyombo vya habari, na jaribio la kuwashinikiza wapiga kura yanakwenda kinyume na makubaliano ya msingi katika kuunda serikali ya umoja wa kitaifa uliofikiwa nchini Arusha,” amesema Bi. Nauert kwenye taarifa yake aliyoitoa jana kwa Vyombo vya Habari.

Burundi iliingia katika makubaliano ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa ili kuondoa machafuko ya vita ya wenyewe kwa wenyewe kati ya Wahutu na Watutsi. Na kwa mabadiliko ya sasa ya Katiba yataruhusu nchi hiyo kuwa na Waziri Mkuu.

Mwezi uliopita Burundi ilifungia mashirika ya habari ya kimataifa ya BBC na VoA kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kukiukwa kwa misingi ya sheria za matangazo.
Rais Nkurunziza kuiongoza Burundi hadi mwaka 2034 Rais Nkurunziza kuiongoza Burundi hadi mwaka 2034 Reviewed by Zero Degree on 5/22/2018 09:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.