Loading...

Nyota Ubelgiji atangaza kustaafu baada ya kuachwa nje ya kikosi cha Kombe la Dunia


Kiungo wa klabu ya Roma na timu ya taifa ya Ubelgiji, Radja Nainggolan ametangaza kustaafu kuichezea timu yake ya taifa baada ya Roberto Martinez kumuacha nje ya kikosi kitakachiobeba Ubelgiji kwenye Kombe la Dunia 2018.

Kwenye ukurasa wake wa Instagram, Radja aliandika hivi:

“Nasita kutangaza kwamba, maisha yangu ya soka la kimataifa yemefika mwisho,

“Nimefanya kila lililowezekana kufanya, kuiwakilisha nchi yangu.

Radja Nainggolan
“Siku zote ukisimamia unachokiamini, inaboa sana. Kuanzia sasa nitakuwa shabiki wa kwanza wa timu yangu ya taifa.”

Martinez alijibu kwa kusema:

“Jambo la kwanza na la msingi, wote tunatambua Radja ni mchezaji mzuri, hakuna swali juu ya hilo.”

“Ni sababu ya kiufundi, wote tunatambua kwamba alikuwa mhimili wa timu kati ngazi ya klabu na sidhani kama tunaweza kumpa majukumu hayo kwenye timu ya taifa.

“Jana (Jumapili) nilisafiri kwenda kumuona Roma na tulikuwa na mazungumzo mazuri. Uamuzi huu haukuwa rahisi, naelewa ni jinsi gani mchezaji huyu alivyomaarufu, lakini tunatakiwa kutengeneza timu iwe tujaribu kuwa timu ya ushindi.

“Hivyo, ni uamuzi wa kiufundi hakuna jambo jingine.”
Nyota Ubelgiji atangaza kustaafu baada ya kuachwa nje ya kikosi cha Kombe la Dunia Nyota Ubelgiji atangaza kustaafu baada ya kuachwa nje ya kikosi cha Kombe la Dunia Reviewed by Zero Degree on 5/22/2018 09:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.