Ikulu yathibitisha uwepo wa Rais Magufuli
Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa asubuhi ya leo Mei 19, 2018 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais- Ikulu, Gerson Msigwa kupitia ukurasa wake maalum wa twitter na kusema Rais Dkt. Magufuli ataungana na wanamichezo katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Tukio hili la kimichezo ni kwa Rais Dkt. Magufuli ndio la kwanza kulifanya tokea alipoingia madarakani na hivyo atakuwa amewawekea historia kubwa klabu ya Simba SC kukabidhiwa kikombe na Rais pamoja na Serengeti Boys.
"Mhe. Rais Magufuli leo ataungana na wanamichezo kupokea kombe la ubingwa wa CECAFA kutoka timu ya Serengeti Boys, kuipokea timu ya TSC iliyoibuka mabingwa wa pili wa dunia huko Urusi na kukabidhi kombe kwa Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kuanzia saa 8 mchana", imesema taarifa ya Msigwa.
Tukio hili la kimichezo ni kwa Rais Dkt. Magufuli ndio la kwanza kulifanya tokea alipoingia madarakani na hivyo atakuwa amewawekea historia kubwa klabu ya Simba SC kukabidhiwa kikombe na Rais pamoja na Serengeti Boys.
Ikulu yathibitisha uwepo wa Rais Magufuli
Reviewed by Zero Degree
on
5/19/2018 08:35:00 AM
Rating: