Loading...

Liverpool wanaongoza mbio za kumsajili beki huyu

Meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp
Tangu Jurgen Klopp achukue madaraka katika klabu ya Liverpool mwaka 2015, timu imeboresheka mno chini ya uongozi wake. Amewaongoza wekundu hao kufika fainali ya kwanza ya michuano ya Ulaya tangu mwaka 2007 kwa kuwafikisha fainali ya Ligi ya Europa mwaka 2016.

Msimu huu, vigogo hao wa Liverpool wamevuka matarajio ya watu wote na safu yao ya mbele inayowajumuisha Sadio Mane, Roberto Firmino na Mohamed Salah wamekuwa wakifunga magoli kwa ajili ya kujifurahisha. Wameisaidia timu kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa, wataikabili Real Madrid tarehe 26 Mei.
Kiungo wa RB Leipzig, Naby Keita anatarajiwa kutua Anfield kwenye majira ya joto lakini Klopp anapanga kufanya usajili mkubwa kukiongezea nguvu kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao.

Wekundu hao wana nia ya kumsajili Diogo Leite kutoka Porto kwenye majira ya joto. Beki huyo wa kati amekuwa akichunguzwa na klabu hiyo ya Uingereza na kiwango cha mreno huyo kimewavutia msimu huu.

Diogo Leite
Kwa mujibu wa taarifa ya The Guardian, kuna klabu nyingine za Ligi Kuu ya Uingereza zinavutiwa na uwezo wake. Liverpool wana matumaini ya kuwapiku wapinzani wao, Arsenal na Manchester City na hatimaye wamsajili Diogo Leite.

Washika bunduki wanaripotiwa kuwa tayari kulipa pauni milioni 13.23 ambazo zinahitajika, lakini wanaweza kumkosa chipukizi huyo mwenye umri wa miaka 19, huku Anfield ikionekana kuwa ndio itakayokua klabu yake mpya.
Liverpool inajenga sifa kubwa kwa kuendeleza vipaji vya wachezaji chipukizi chini ya kocha kutoka Ujerumani na hilo linaweza kuwasaidi kuzipiku Arsenal na Manchester City. Kama dili hilo litakamilika wanampango wa kumtoa kwa mkopo ili apate muda mwingi wa kucheza na kikosi cha kwanza.
Liverpool wanaongoza mbio za kumsajili beki huyu Liverpool wanaongoza mbio za kumsajili beki huyu Reviewed by Zero Degree on 5/10/2018 07:01:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.