Loading...

Nyota huyu wa PSG anaweza kutua Bernabeu baada ya Kombe la Dunia

Wachezaji wa Paris Saint-Germain, Edison Cavani (Uruguay), Neymar Jr (Brazil) na Kylian Mbappe (Ufaransa)

Neymar alijiunga na Paris Saint-Germain akitokea Barcelona kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 200, ambayo ilivunja rekodi ya usajili mwezi Agosti mwaka jana. Mbrazili huyo alijiunga na vigogo wa La Liga mwaka 2013 na kufurahia kipindi cha mafanikio pale lakini aliamua kuondoka kwani hakutaka kuendelea kucheza chini ya kivuli cha Lionel Messi na kutaka kujitegemea.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 alikuwa kwenye kiwango chake cha juu akiwa na vigogo hao wa Ufaransa, akifunga magoli 28 na kutoa 'assist' 16 katika mechi 30 kabla hajaingia majeruhi. Alienda Brazil kwa matibabu na sasa amerejea Paris wikendi hii kuanza hatua ya mwisho ya matibabu yake.

Lakini kwa mujibu wa ripoti mbalimbali, mshambuliaji huyo hajayafurahia maisha ya Paris licha ya kwamba hajatimiza hata mwaka mmoja akiwa katika mji mkuu wa Ufaransa. Amekua akihusishwa sana na uhamisho kwenda Real Madrid kwenye majira ya joto, ikiaminika kwamba anataka kucheza pamoja na Cristiano Ronaldo.
Real Madrid pia wanatarajiwa kuimarisha kikosi chao kwenye majira ya joto na wanaweza kujaribu kumsajili Mbrazil, kama ataamua kuondoka.
Aliyekuwa kiungo wa Barcelona, Edmilson anaamini kuna uwezekano mkubwa wa Neymar kwenda Real Madrid baada ya Kombe la Dunia.

Kwa mujibu wa taarifa ya El Larguero, Edmilson alisema: “Nilishangaa kuona Neymar anaondoka Barcelona, lakini hiyo ni juu yake yeye pamoja na timu yake.”

“Sitashangaa sana kama, baada ya Kombe la Dunia, Neymar atajiunga na Madrid.”
Nyota huyu wa PSG anaweza kutua Bernabeu baada ya Kombe la Dunia Nyota huyu wa PSG anaweza kutua Bernabeu baada ya Kombe la Dunia Reviewed by Zero Degree on 5/06/2018 02:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.