Real Madrid watalenga kumsajili nyota huyu kama watashindwa kwa Neymar
Neymar aliungana na wenzake kwenye sherehe za Ubingwa wa Ligi Kuu ya Ufaransa |
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 alikuwa kwenye kiwango chake cha juu akiwa na vigogo hao wa Ufaransa, akifunga magoli 28 na kutoa 'assist' 16 katika mechi 30 kabla ya majeruhi. Alienda Brazil kwa matibabu lakini amesharejea Paris na anaendelea na hatua ya mwisho ya matibabu yake.
Lakini kwa mujibu wa ripoti mbalimbali, mshambuliaji huyo hajayafurahia maisha ya Paris licha ya kwamba hajatimiza hata mwaka mmoja akiwa katika mji mkuu wa Ufaransa. Amekua akihusishwa sana na uhamisho kwenda Real Madrid kwenye majira ya joto, ikiaminika kwamba anataka kucheza pamoja na Cristiano Ronaldo.
Real Madrid pia wanatarajiwa kuimarisha kikosi chao kwenye majira ya joto baada ya kufanya vibaya kwenye La Liga msimu huu. Klabu hiyo inataka kusajili mchezaji mwenye uwezo mkubwa na Mbrazil huyo ni chaguo lao la kwanza, huku Florentino Perez akiamini ana uwezo wa kumudu gharama zake kwenye majira ya joto.
Lakini klabu hiyo inayoongozwa na Zinedine Zidane inatambua kwamba PSG haitamwachia nyota huyo kiurahisi na wameanza kuchukua hatua nyingine kama watashindwa kumnasa.
Paulo Dybala |
Wakati Neymar akiendelea kubakia kuwa chaguo la kwanza la Real Madrid kwenye usajili wa majira ya joto, mshambuliaji wa Juventus, Paulo Dybala ameibuka na kuwa chaguo lao la pili, kwa mujibu wa taarifa ya Don Balon.
Dybala amekuwa kwenye kiwango cha hali ya juu sana msimu huu, akifanikiwa kufunga magoli 22 kwenye Ligi Kuu ya Italia. Lakini yuko kwenye mgogoro na Massimiliano Allegri, pia amekuwa na shida nyingine zinazomtatiza mara kadhaa nje ya uwanja na amekuwa akihusishwa na kuondoka Italia kwenye majira ya joto.
Vigogo hao wa Serie A hawataki kumuuza Mwajentina huyo na wanaweza kumpa ofa ya mkataba mpya utakaoambatana na ongezeko kubwa kwenye mashahara wake wa sasa kumfanya aachane na vilabu vingine. Licha ya kuwa na kuwa na kiwango kinachopanda na kushuka bado wana imani anaweza kuwa mchezaji muhimu sana kwenye mafanikio yao ya baadaye.
Real Madrid bado wana nia ya kujaribu kumsajili nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 kama watashindwa kumsajili aliyekuwa nyota wa klabu ya Barcelona. Lakini watakabiliwa na ushindani kutoka Bayern Munich, Barcelona na Atletico Madrid kwenye kuwania saini ya Mwajentina huyo.
Real Madrid watalenga kumsajili nyota huyu kama watashindwa kwa Neymar
Reviewed by Zero Degree
on
5/21/2018 12:50:00 PM
Rating: