Loading...

Spika Ndugai aibana koo Serikali


Spika Job Ndugai ameitaka Serikali kutoa majibu ya tofauti ya bei ya sukari kati ya Tanzania Bara na Zanzibar, ambapo Tanzania bara bei ni maradufu na kusema suala hilo haliwezekani hata kidogo.

Akihitimisha mjadala wa sukari ambao haukupatiwa majibu, Spika Ndugai amesema kwamba swali lililoulizwa na Wabunge akiwepo Mbunge wa Mpendae, Tuky ni la msingi sana na bado halijapatiwa majibu hivyo kuamua kulipanga wiki ijayo.

Kama ni kweli wananchi wa Tanzania bara wanalipa sukari mara mbili ya ya Zanznibar ili tu kulinda wenye viwanda....Haiwezekeni hiyo. Bunge linahitaji majibu ya uhakika.

Kumekuwa na mvutano bungeni kuhusu bei ya sukari katika viwanda vya Tanzania bara kuuzwa bei ghali kuliko Zanzibar jambo ambalo Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage amesema hiyo ni kutokana na gharama za uzalishaji bara kuwa juu kuliko Zanzibar.
Spika Ndugai aibana koo Serikali Spika Ndugai aibana koo Serikali Reviewed by Zero Degree on 5/08/2018 10:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.