Loading...

Mwamuzi atakayechezesha fainali ya Ligi ya Mabingwa kati ya Liverpool na Real Madrid

Cristiano Ronaldo (katika) akilalamikia uamuzi wa Mazic wakati Ureno ilipochapwa bao 4-0 na Ujerumani mwaka 2014
Milorad Mazic amechaguliwa na UEFA kuchezeshe fainali ya Ligi ya Mabingwa kati ya Liverpool na Real Madrid mjini Kiev tarehe 26 Mei.
Cristiano Ronaldo anaweza asiupokee vizuri uchaguzi huo utakaomkutanisha tena na mwamuzi ambaye alikosolewa sana kwa maamuzi yake yenye utata yaliyochangia kutolewa kwa Ureno kwenye Kombe la Dunia mwaka 2014.

Ronaldo alionyesha kuchukizwa na uamuzi wake wakati Ureno ilivyochapwa bao  4-0 na ujerumani mwaka 2014 — ndani ya mchezo huo, aliyekuwa beki wa Real Madrid, Pepe alitolewa nje baada ya Mario Gotze kuzawadiwa penalti kwa rafa ya wazi aliyocheza Joao Pereira.

Milorad Mazic atachezeshe fainali ya Ligi ya Mabingwa kati ya Liverpool na Real Madrid mjini Kiev, tarehe 26 Mei
Mazic aliichezesha Real Madrid msimu uliopita, akimtoa 
Timothee Kolodziejczak wa Sevilla kabla vijana wa Zinedine Zidane hawajashinda UEFA Super Cup kwa ushindi wa bao 3-2 kwenye muda wa nyongeza.
Ameshachezesha mechi tano kwenye Ligi ya Mabingwa msimu huu, ikiwa ni pamoja na mchezo mmoja wakati wa hatua ya kufuzu. Alitoa kadi za 18 njano kwa wastani wa 3.6 kwa kila mchezo.

Bjorn Kuipers atachezesha fainali ya Ligi ya Europa
Bjorn Kuipers atachezesha fainali ya Europa Ligi tarehe 16 Mei wakati Atletico Madrid watakapokutana na Marseille huko Lyon.
Ni fainali ya pili ya Europa Ligi kwa Kuipers, baada ya kuichezesha Chelsea mwaka 2013 ilipoibuka na ushindi dhidi ya Benfica. Mholanzi huyo pia alichezesha fainali ya Ligi ya Mabingwa 2014, Atletico ilipochapwa na Real Madrid.

Mazic na Kuipers wote wamechaguliwa na FIFA kuchezesha kwenye Kombe la Dunia kwa mara ya pili mfululizo, ambalo linaanza mwezi ujao.
Mwamuzi atakayechezesha fainali ya Ligi ya Mabingwa kati ya Liverpool na Real Madrid Mwamuzi atakayechezesha fainali ya Ligi ya Mabingwa kati ya Liverpool na Real Madrid Reviewed by Zero Degree on 5/08/2018 07:46:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.